Monday , 11 December 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Ujenzi shule ya kwanza kata ya Kilimani washika kasi
Elimu

Ujenzi shule ya kwanza kata ya Kilimani washika kasi

Spread the love

HATIMAYE kata ya Kilimani katika Jiji la Dodoma imeanza ujenzi wa shule ya msingi itakayogharimu kiasi cha Sh 80 milioni kwa kuanza na vyumba vinne vya madarasa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Ujenzi huo wa shule ya msingi unatokana na kata hiyo kutokuwa na shule ya msingi wala  sekondari tangu kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika.


Hali hiyo inatajwa kusababisha watoto kutembea umbali wa kilomita tatu kusaka elimu katika vijiji jirani.

Hata hivyo, leo tarehe 11 Oktoba 2023 Viongozi wa Kamati ya siasa ya  Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kilimani Jijini Dodoma pamoja na Wajumbe wa  Sekretarieti   ya kata ya kilimani wamefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa Shule  ya Msingi  unaotekelezwa katika Mtaa wa Chinyoyo.

Pamoja na kasi ya ujenzi huo  unaoendelea  viongozi hao wamesisitiza kasi katika ujenzi huo ili ukamilike kwa haraka na kwa wakati.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani, Nathani Chibeye amesema ujenzi huo wa shule ya msingi utakuwa mkombozi kwa kata ya kilimani na kuondoa adha ya watoto kutembea umbali mrefu kwenda shule za jirani.

Kwa upande wake Katibu wa CCM kata ya Kilimani, Rotta Ndimbo ameitaka kamati ya ujenzi na mkandarasi kuhakikisha wanatanguliza uzalendo katika ujenzi wa shule hiyo ili thamani ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo zitumike kama zilivyo kusudiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuTangulizi

Mwalimu Maganga Japhet asimamishwa kazi kwa utoro

Spread the loveMwalimu Maganga Japhet amesimamishwa kazi na Tume ya Utumishi wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

CEO NMB awataka vijana kunoa ujuzi wao

Spread the loveAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, amewashauri...

Elimu

150 wahitimu Shahada ya Udaktari HKMU

Spread the loveCHUO Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), kimeiomba serikali...

Elimu

Aliyehitimu udaktari HKMU na miaka 21 atoa siri

Spread the love MHITIMU wa fani ya udaktari ambaye ni mdogo kuwahi...

error: Content is protected !!