Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Biashara Mgogoro wa wachimbaji Mafurungu watatuliwa, wapewa leseni
BiasharaHabari Mchanganyiko

Mgogoro wa wachimbaji Mafurungu watatuliwa, wapewa leseni

Spread the love

Serikali kupitia Wizara ya Madini imetatua rasmi mgogoro wa wachimbaji wadogo wa madini uliodumu kwa mwaka mmoja katika Kitongoji cha Mafurungu – Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza jana Jumanne katika Mkutano na wachimbaji wadogo Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema Serikali kupitia  Wizara ya Madini inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika ukuaji wa uchumi wa taifa hivyo inafanya kila juhudi ili kuona wachimbaji wadogo wa madini wapo katika mazingira salama ya uchimbaji.

Mavunde amefafanua kuwa maana ya mazingira bora ya uchimbaji ni pamoja usalama katika uchimbaji, kuchimba kwa kutumia vifaa vya kisasa lakini pia kuwa na taarifa sahihi za uwepo wa madini ili kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha.

“Kutokana na umuhimu wanu katika sekta ya madini leo tunafunga rasmi mgogoro  kwa kuwapatia leseni nne za uchimbaji ili kila mmoja achimbe  bila kuwepo na mgogoro wowote  katika kitongoji cha Mafurungu,” amesema.

Sambamba na hapo Mavunde ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wachimbaji  katika maeneo yao ya kazi ambapo katika juhudi za kuunga mkono maendeleo ya kitongoji cha Mafurungu  tayari ametoa ahadi ya mifuko 200 ya Saruji na kuwa Balozi wa kujitolea kwa eneo hilo.

Naye, Kamishna wa Madini Dk. AbdulRahm Mwanga ameupongeza uongozi wa Wachimbaji Wadogo wa madini kupitia Chama Cha Wachimbaji Wadogo Mafurungu (UWAWAMA) kwa kukubali na kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri wa Madini na kuweza kufuta  sintofahamu zote zilizokuwepo awali.

Awali , Meneja Mgodi  Mbwana Mosses  akisoma taarifa ya  mafanikio ya Chama cha UWAWAMA kuhusu uzalishaji wa dhahabu amesema kuwa hadi sasa chama kupitia migodi yake kimeweza kuzalisha kiasi cha gramu 11093.19 za dhahabu ambazo zina thamani yaSh 1.3 bilioni na kulipa Mrabaha wa Sh. 80 milioni.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Mvumi Livingstone Lusinde, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Afisa Madini Mkazi Dodoma,Viongozi wa Dini na wachimbaji wadogo madini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!