WATU zaidi ya 10 katika Wilaya ya Kyotera, nchini Uganda, wameripotiwa kupoteza maisha kwa mlipuko wa ugonjwa usiojulikana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).
Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, Wizara ya Afya nchini Uganda, wamechukua sampuli za miili ya waliofariki dunia kwa ajili ya kuchunguza mlipuko huo unaotajwa kutokea ndani ya wiki mbili zilizopita.
Imeripotiwa kuwa, wahanga wa mripuko huo wamebainika kupatwa na vipele mwilini, kuvimba baadhi ya viungo vya mwili, kabla ya kupoteza maisha.
Wizara ya Agya Uganda imewataka wananchi wanapopatwa na dalili hizo kuripoti kwenye vituo vya afya badala ya kwenda kwa waganga wa kienyeji, ili Serikali iweze kuudhibiti.
Leave a comment