NCHI ya Israel, pamoja na kikundi cha wanamgambo wa kiislamu, Hamas, wamekubaliana kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza, ili kuruhusu zoezi la kuacha huru mateka wa pande zote mbili. Inaripoti Mtandao ya Kimataifa…(endelea).
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, uamuzi huo wa kusitishwa kwa mapigano kwa muda wa siku nne mfululizo ili kutoa nafasi ya mateka wa pande zote mbili kuachwa huru, unafuatia hatua ya Serikali ya Israel kuidhinisha mpango wa kuwaacha huru mateka wa Palestina zaidi ya 150, wakiwemo wanawake na watoto.
Kwa upande wa Hamas, umetoa taarifa iliyodai kwamba, endapo wapalestina 150 wataachwa huru kutoka katika jela za Israel, chini ya makubaliano maalum, watawaachia mateka wa Israel 50.
Mbali na kubadilishana mateka, makubaliano hayo yametajwa kuruhusu uingizaji wa malori yanayobeba misaada ya kibinadamu, vifaa vya matibabu na mafuta, kuingia upande wa Gaza.
Uamuzi wa kuachwa huru mateka, unajiri baada ya Shirika linalotetea haki za binadamu, Human Right Watch, kudai takribani wapalestina 7,000 wakiwemo wanawake na watoto wanazuiliwa katika magereza ya Israel, huku wakihojiwa bila kupata uwakilishi wa kisheria.
Kwa sasa mitandao ya kimataifa imeripoti kuwa, majeshi ya Israel yanaendelea kuishambulia Gaza.
Leave a comment