Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Uchaguzi Nigeria waahirishwa; Buhari, Abubakar kusubiri hukumu
Kimataifa

Uchaguzi Nigeria waahirishwa; Buhari, Abubakar kusubiri hukumu

Spread the love

UCHAGUZI wa rais nchini Nigeria uliopangwa kufanyika leo tarehe 16 Februari 2019, umeahirishwa. Vinaripoti vyombo vya habari vya kimataifa…(endelea).

Taarifa zaidi kutoka katika Tume Huru ya Kitaifa Uchaguzi ya Nigeria (INEC) zinasema kuwa, sababu kubwa ni kutokamilika mpango mzuri wa kufanyika uchaguzi huo ili kuepuka manung’uniko.

Kutokana na tangazo hilo, wagombea 73 wanaowania urais watalazimika kusubiri akiwemo anayetetea kiti chake Rais Muhammadu Buhari (76) anayechuana vikali na mpinzani wake mkuu, aliyekuwa makamu wa rais Atiku Abubakar (72).

Uchaguzi wa urais na ubunge nchini humo sasa utafanyika Jumamosi ijayo ya tarehe 23 Februari 2019. INEC ilitangaza hairisho hilo saa tano kabla ya wananchi kwenda kwenye foleni kwa ajili ya kupiga kura.

Mahmood Yakubu, Mwenyekiti wa INEC alisema kuwa, kuna hitilafu za mpango uliowekwa wa ajili ya kufanya uchaguzi huo na sasa, unafanyiwa kazi ili wiki ijayo uchaguzi huo ufanyike.

“Uamuzi huu umelenga kuhakikisha uchaguzi unafanyika na kuwa huru na haki. Sasa uchaguzi utafanyika tarehe 23 Februari mwaka huu,” alisema Yakubu.

Kwenye tangazo lake hilo alisema, uchaguzi wa Ugavana, wawakilishi wa majimbo na mabaraza ya manispaa utafanyika wiki mbili baada ya uchaguzi wa rais (9 Machi 2019).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Ayatollah Khamenei aongoza wairan kumuaga Raisi

Spread the loveKiongozi wa Juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, ameongoza mjini...

AfyaKimataifaTangulizi

Waliowekewa damu yenye VVU, homa ya ini kulipwa fidia trilioni 32.9

Spread the loveWaziri mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak ameahidi kulipa fidia ya...

Habari za SiasaKimataifa

Balozi Kasike ateta na mjumbe wa FRELIMO

Spread the loveBalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine...

Kimataifa

Zuma akwaa kisiki, mahakama yamzuia kuwani urais

Spread the loveMahakama ya katiba nchini Afrika Kusini, katika uamuzi wake imesema...

error: Content is protected !!