Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kubenea atoa neno zito, agawa madawati
Habari za SiasaTangulizi

Kubenea atoa neno zito, agawa madawati

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo akikata utepe ishara ya kukabishi madawati katika shule ya Sekendari ya Mashujaa, iliyopo Sinza
Spread the love

MBUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, amekabidhi madawati 290 yatakayotumika katika shule za Msingi na Sekondari katika jimbo hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Madawati hayo yalikabidhiwa leo, tarehe 15 Februari, katika hafla iliyofanyika kwenye Shule ya Sekondari Mashujaa, iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na walimu, wanafunzi, kamati ya shule, wazazi na baadhi ya wananchi wa eneo hilo na maeneo mengine jirani, Kubenea alisema, ameamua kuchangia madawati hayo ili kusaidia wanafunzi hao kupata elimu bora ya maisha yao.

Amesema, “nimekuja hapa kutoa madawati haya, siyo kwa sababu fedha za mfuko wa jimbo hazina kazi nyingine. Hapana. Nimefanya hivyo kutokana na kuona jimbo la Ubungo, lina matatizo makubwa ya madawati.”

Alisema, “mlinichagua ili kuwa mwakilishi wenu kwa serikali na kusaidia utatuzi wa matatizo yaliyopo kwenye jamii. Kutokana na dhamira hiyo, nimeona kuna umuhimu mkubwa wa kusaidia matatizo yetu katika sekta ya elimu kwenye shule zetu.”

Shule ya Sekondari Mashujaa, ni miongoni mwa shule sita za Sekondari zilizopo jimbo la Ubungo ambazo zimepatiwa msaada wa madawati hayo.

Shule nyingine ambazo zitapata madawati, ni Shule ya Sekondari Makoka, Mugabe, Mabibo, Manzese na Makurumla.

Kwa upande wa shule za Msingi, Kubenea alizitaja shule hizo kuwa ni Ubungo Plaza, Muungano na Golani B. Madawati yaliyokabidhiwa yamenunuliwa na fedha kutoka mfuko wa jimbo.

Katika hatua nyingine, mbunge huyo amekemea tabia ya baadhi ya viongozi ya kutumia fedha za mfuko wa jimbo kwa manufaa yao binafsi.

Ametolea mfano kata ya Sinza ambako kulipelekwa takribani Sh. 3 milioni kwa ajili ya kusaidia vikundi vya wanawake, lakini fedha hizo hazikufika kwa walengwa.

“Hapa Sinza nilitenga na kuzileta kiasi cha Sh. 3 milioni kwa ajili ya kusaidia vikundi vya wanawake kupata maendeleo. Lakini nasikitika sana, kwamba fedha hizo hazikufika kwa walengwa. Taarifa nilizonazo, fedha zile zimepigwa na wajanja wachache pale kwenye ofisi ya mtendaji kata,” ameeleza Kubenea kwa sauti ya masikitiko.

Hata hivyo, Kubenea amesema, fedha za serikali haziwezi kuliwa kama shamba la bibi, hivyo atafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa wote waliohusika na wizi huo, wanachukuliwa hatua kali za kisheria.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mashujaa, Edda Kondo, akizungumza katika hafla hiyo, alimshuruku mbunge kwa msaada alioutoa na kuahidi kuyatunza na kuyalinda madawati hayo.

Alisema, “tunakushuru sana kwa msaada huu. Tunakuahidi tutaulinda na kuutangaza.”

 Aliongeza: “Tukumbuke kuwa Tanzania yetu ya Viwanda na teknolojia haiwezi kufika, bila kuwa na maabara zenye vitendea kazi thabiti kwa ajili ya matumizi ya ofisi kama kuchapia mitihani. Tunakuomba na hili uliangalie.”

Aidha, Mwalimu Kondo alimuomba mbunge huyo kusaidia shule yake ukarabati wa vyumba vya madarasa 17, maabara, vifaa vya sayansi na ofizi za walimu.

Kubenea alisema, amepokea maombi hayo na atayafanyia kazi kwa kadri fedha zitakapopatikana. Aliahidi kutumia fedha za mfuko wa jimbo na misaada kutoka kwa marafiki zake, kufanikisha mambo hayo.

Kwa upande wake, Afisa Elimu Sekondari, Hilda Shalanda aliyeongea kwa niaba ya mkurugenzi wa manipaa ya Ubungo alisema, alimshukuru mbunge Kubenea kwa kusikiliza kilio chao cha kukabiliana na matatizo ya madawati.

Alisema, “kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa ya Ubugo, tunakushuruku sana kwa msaada huu. Tunakushuru pia kwa ahadi yako ya kusaidia tena shule hii na shule nyingine zilizopo katika jimbo lako. Mungu akubariki.”

Mbali na kukabidhi madawati hayo, Kubenea alitembelea kata ya Kimara ambako alikagua ujenzi wa uzio katika shule ya Msingi Golani B na kutembelea mradi wa maji ambao umefadhiliwa na ofisi ya mbunge.

Akiwa Kimara, Kubenea alieleza masikitiko yake ya jinsi ya ofisi ya Kata ilivyoshindwa kumalizia mradi wa maji ambao ulilenga kupeleka huduma kwa wananchi na wanafunzi wa shule hiyo.

Aliahidi kutenga kiasi kingine cha fedha kumaliza mradi huo na kukemea kitendo cha mmoja wa maofisa wa serikali anayedaiwa kutafuna baadhi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Katika ziara hiyo, Kubenea aliongozana na baadhi ya madiwani, maofisa watendaji kata, maofisa kutoka manispaa ya Ubungo na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya Chadema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

error: Content is protected !!