BARAZA la Mitihani la Tanzania limefungia vituo vya mtihani viwili ambavyo ni Twibhoki (PS0904095) na Graiyaki (PS0904122) vyote vya Halmashauri ya Serengeti mkoa wa Mara vilivyothibitika kupanga kufanya udanganyifu katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Said Mohamed amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa mujibu wa Kifungu 4(8) cha Kanuni za Mitihani mwaka 2016 mpaka hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni salama kwa uendeshaji wa Mitihani ya Taifa.
Aidha, baraza hilo pia limeziandikia barua za onyo vituo vya mtihani vinne ambavyo ni Mother of Mercy (PS0203133), St. Marys’ Mbezi Beach (PS0203088) vya Halmashauri ya Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam, Charm Modern (PS0103111) cha Halmashauri ya Karatu mkoa wa Arusha pamoja na Morotonga (PS0904042) cha Halmashauri ya Serengeti mkoa wa Mara.
Amesema vituo hivyo vilijaribu kujihusisha na vitendo vya udanganyifu katika mtihani.
“Vituo hivyo vitakuwa chini ya uangalizi wa Baraza la Mitihani mpaka hapo Baraza litakapojiridhisha kuwa ni vituo salama kwa uendeshaji wa Mitihani ya Taifa,” amesema.
Leave a comment