Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Tinubu awaachisha kazi maofisa wa jeshi, polisi
Kimataifa

Tinubu awaachisha kazi maofisa wa jeshi, polisi

Spread the love

RAIS wa Nigeria, Bola Tinubu amefanya mabadiliko makubwa kwa vikosi vya ulinzi jana Jumatatu na kuwasimamisha kazi wakuu wa usalama na mkuu wa polisi chini ya mwezi mmoja baada ya kuingia madarakani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Tinubu, ambaye aliapishwa tarehe 29 Mei 2023, amefanya sekta ya usalama kuwa moja ya vipaumbele vyake vikuu na kuahidi mageuzi makubwa.

Hiyo ni pamoja na kuajiri askari zaidi na maofisa wa polisi, huku akiwaongezea mishahara bora na kuwapatia vifaa bora zaidi.

Wanajeshi wa Nigeria wamekuwa wakipambana na waasi wa kiislamu kwa muda mrefu katika maeneo ya kaskazini masharik mwa nchi, huku visa vya ujambazi na utekaji nyara kwa lengo la kulipwa fidia, vikiongezeka katika eneo la kaskazini magharibi, wakati ukosefu wa usalama ukienea katika maeneo mengi ya nchi.

Siyo kawaida kwa rais mpya wa Nigeria kuwalazimisha wakuu wa usalama kustaafu mapema baada ya kuchukua madaraka, kama Tinubu alivyofanya Jumatatu.

Alimchagua Nuhu Ribadu, afisa mkuu wa zamani wa polisi na mkuu wa zamani wa mamlaka ya kupambana na uhalifu wa kiuchumi na kifedha nchini humo, kama Mshauri wake wa Usalama wa Kitaifa.

Meja Jenerali Christopher Musa, ambaye hadi mwaka jana alikuwa akiongoza mapambano ya jeshi dhidi ya waasi, anachukua nafasi ya mkuu mpya wa majeshi kutoka kwa Lucky Irabor. Tinubu pia aliwateua makamanda wapya wa jeshi la ardhini, la wanamaji na la anga pamoja na mkuu mpya wa Huduma ya Forodha ya Nigeria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!