November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tanzania, Kenya, Ethiopia, Nigeria zapigwa ‘Stop’ kuingia UAE kisa Corona

Spread the love

 

UMOJA wa Falme za Kiarabu (UAE), zimesitisha safari za ndege kwa abiria wanaotoka nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia na Nigeria, huku ikiongeza vikwazo vya usafiri kwa abira wa Uganda na Ghana. Unaripoti Mtandao wa BBC Swahili … (endelea).

Kwa mujibu wa mtandao huo, agizo hilo litaanza kutekelezwa usiku wa tarehe 25 Desemba 2021, ambapo chanzo cha sitisho la safari za ndege kwa nchi hizo, kikitajwa ni kudhibiti usambaaji wa Ugonjwa wa Virusi vya Corona (UVIKO-19-19).

Marufuku hiyo ilitolewa jana Alhamisi, tarehe 23 Desemba 2021 na Mamlaka ya Kudhibiti Dharura na Majanga UAE (NCEMA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini humo (GCAA).

Kwa mujibu wa mitandao ya kimataifa, watu watakaoruhusiwa kuingia katika umoja huo ni, raia wake, wanadiplomasia na wajumbe maalum kati ya nchi hizo na UAE.

Watu hao walioruhusiwa kuingia UAE wamepewa masharti kadhaa, ikiwemo kuwasilisha majibu ya vipimo yanayoonesha hawana UVIKO-19, vipimo hivyo vifanyike ndani ya saa 48.

Pamoja na kupimwa tena wakiwa katika uwanja wa ndege, ndani ya saa sita kabla ya safari kuanza.

Hata hivyo, safari za ndege kutoka UAE kwenda katika mataifa hayo zitaendelea kama kawaida.

error: Content is protected !!