Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Michezo Mmewasikia KMC, wataka kuwapa mashabiki wao zawadi ya Krisimasi
Michezo

Mmewasikia KMC, wataka kuwapa mashabiki wao zawadi ya Krisimasi

Spread the love

 

KLABU ya KMC ya Kinondoni inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imetamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba, ili iwe kama sehemu ya zawadi ya sikukuu ya Krisimasi kwa mashabiki wa timu hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa duru la kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara utapigwa hii leo majira ya saa 10 kamili jioni kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi, mkoani Tabora.

Akizungumza na Raia Mwema kuelekea mchezo huo Afisa Habari wa KMC, Christina Mwangala amejitanabaisha kuwa mchezo huo utakuwa mgumu lakini pia mwepesi kutokana na walivyojiandaa na wanataka kutumia matokeo ya mchezo huo kama zawadi ya sikukuu ya Krisimasi kwa mashabiki wa timu yao.  

“Mchezo wa kesho ni mguu lakini mwepesi, ni mechi ambazo wachezaji wamezizoea na kila mmoja anajiandaa kwa namna yake, ni mechi nzuri na kuvutia tunahitaji kuwapa mashabiki wetu zawadi ya Christmas na mwaka mpya,” alisema Afisa habari huyo.

Kikosi hiko kinaingia kwenye mchezo huo, huku kikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bila kufungana kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Katika michezo mitano iliyopita ya Ligi Kuu Tanzania Bara, KMC haijapoteza mchezo hata mmoja na kushinda michezo mitatu, huku ikienda sare mara mbili.

Kikosi cha Simba kikifanya mazoezi

Aidha msemaji huyo aliendelea kusema kuwa mpaka sasa kikosi chao hakuna changamoto yoyote ya maradhi yaliyoibuka hivi karibuni.

“Kwetu sisi changamoto tulipitia kwenye mechi zaidi ya Mtibwa Sugar, lakini hatukuweka wazi na wachezaji waliweza kukava na tukacheza mechi na Mtibwa lakini mpaka sasa hakuna anayeumwa,” alisema Afisa Habari huyo.

Kikosi cha Kmc kiliwasili mkoani Tabora siku ya jana na kufanya maandalizi ya mwisho kuwakabili mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!