January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sure Boy kwenye rada za Yanga

Spread the love

MARA baada ya kupewa mkono wa kwaheri kwenye klabu yake ya Azam FC, kiungo Salum Abubakar “Sure Boy” huenda muda wowote kuanzia sasa akatangazwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Yanga, kwenye dirisha hili dogo la usajili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Sure Boy ambaye amedumu ndani ya Azam FC kwa miaka 13 toka timu hiyo ilipokuwa Ligi Daraja la kwanza, aliandikia uongozi wa timu hiyo barua ya kuvunja mkataba wake mara baada ya kusimamishwa kwa kipindi kisichojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.

Mchezaji huyo alisimamishwa sambamba na wachezaji wengine waandamizi wa klabu hiyo, akiwemo mkongwe na nahodha wa muda wote wa kikosi hicho, Aggrey Morris pamoja na Mudathiri Yahaya licha ya hivi karibuni kusamehewa na kurejea kikosini.

Mara baada ya kupewa baraua rasmi na uongozi wa Azam FC kuonesha kukubaliana na ombi lake la kuvunja mkataba, vyanzo vya kuamika kutoka kwa watu wake wa karibu pamoja na kutoka ndani ya Yanga, vimeeleza kuwa tayari mchezaji huyo yupo kwenye hatua za mwisho kutambulishwa kama mcheaji mpya ndani ya klabu hiyo.

Moja ya chanzo hiko kilieleza kuwa tayari ameshasaini kandarasi ya miaka miwili kuwatumikia vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo.

“Sure Boy amesaini miaka miwili na Yanga, hivyo muda wowote kutoka sasa watamtambulisha.” Kilieleza chanzo hiko.

error: Content is protected !!