January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Timu 10 kukiwasha Mapinduzi, Simba na Yanga…

Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini

Spread the love

 

MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi 2021 visiwani Zanzibar, itaanza tarehe 2 hadi 13 Januari huku timu kumi zikithibitisha kushiriki ikiwemo bingwa mtetezi Yanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Michuano hiyo hufanyika kila mwaka kusherekea Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika tarehe 12 Januari 1964. Mwaka huu inatimia miaka 58 ya Mapinduzi.

Katika michuano hiyo, timu nne ni za Tanzania Bara ambazo ni Simba, Yanga, Namungo na Azam FC pamoja na sita za Zanzibar.

Kikosi cha Simba kikifanya mazoezi

Timu hizo zimegawanywa kwenye makundi matatu ya timu tatu tatu na kundi moja likiwa na timu nne.

Kundi A lina timu za Azam FC, Namungo FC, Yosso Boys na Meli City.

Kundi B kuna bingwa mtetezi Yanga, Taifa Jang’ombe na KMKM.

error: Content is protected !!