January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Taliban wapiga marufuku fedha za kigeni Afghanistan

Spread the love

 

Kundi la Taliban limetangaza kupiga marufuku matumizi ya fedha za kigeni nchini Afghanistan hatua ambayo inazidi kuongeza mdororo wa uchumi nchini humo tangu kundi hilo kutwaa madaraka Agosti mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Tangazo hilo la kushangaza limetolewa jana tarehe 2 Novemba mwaka huu ikiwa ni saa chache baada ya kutokea shambulio la bomu na milio ya risasi katika hospitali kubwa ya kijeshi jijini la Kabul nchini humo.

Shambulio hilo limesababisha vifo vya watu 19 akiwamo mwanamgambo mmoja wa Taliban pamoja na maelfu ya majeruhi.

Taarifa iliyotumwa mtandaoni na msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid imesema; “Jamhuri ya Kiislamu inawaagiza raia wote, wenye maduka, wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla… wanaofanya shughuli zao hapa nchini Afghanistan, kujiepusha na matumizi ya fedha za kigeni.

“Yeyote atakayekiuka agizo hili atachukuliwa hatua za kisheria,” ilisema taarifa hiyo.

Matumizi ya dola za Marekani yameenea katika masoko ya Afghanistan, wakati maeneo ya mpakani yakitumia sarafu ya nchi jirani kama vile Pakistan kwa biashara mbalimbali.

Serikali ya Taliban inashinikiza kutolewa kwa mabilioni ya dola ya akiba ya benki kuu wakati taifa hilo lililokumbwa na ukame likikabiliwa na uhaba wa pesa, baa la njaa.

Serikali ya awali ya Afghanistan inayoungwa mkono na nchi za Magharibi ilikuwa imehifadhi mabilioni ya dola na mali katika Hifadhi ya Shirikisho la Marekani na benki nyingine za Ulaya.

Lakini baada ya Taliban kuchukua nchi mwezi Agosti, Marekani, Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), waliamua kuzuia upatikanaji wa fedha hizo za Afghanistan zaidi ya dola za marekani bilioni 9.5.

Uamuzi huo umekuwa na athari mbaya katika huduma ya afya nchini humo na sekta nyingine.

error: Content is protected !!