WAGOMBEA wawili katika kinyang’anyiro cha uongozi wa chama cha Conservative leadership wamewasilisha mipango yao kwa wajumbe wa chama ambao watamchagua mrithi wa Boris Johnson. Yanaripoti Mashirika ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa BBC, Rishi Sunak na Liz Truss walipata kura nyingi zaidi katika uchaguzi wa mwisho wa wabunge Jumatano.
Akiandika katika gazeti la Daily Telegraph, Sunak amesema atapanga “mageuzi makubwa kama yale ambayo Margaret Thatcher aliyafanya katika miaka ya 1980”.
Katika Daily Mail, Truss ameahidi “kukata kodi, kuboresha biashara, na kuweka sera rafiki za biashara za Conservative”.
Wawili hao waliibuka kuwa wagombea wakuu baada ya Truss kubadilisha ushindi mdogo wa Waziri wa biashara Penny Mordaunt, ambaye wakati mmoja alipendelewa, kwa kupata uungaji mkono wa Waconsertvative 113 dhidi ya Mordaunt aliyepata 105.
Kansela wa zamani Sunak, ambaye aliendelea kuongoza miongoni mwa wabunge, alishinda kwa kura 137.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa ni mtu ambaye ana umaarufu wa kiwango cha chini zaidi miongoni mwa wajumbe wa chama cha Conservative ambao watapiga kura kwa mgombea ajaye mwezi ujao.
Leave a comment