Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Sunak azidi kuongoza mbio kumrithi Johnson
HabariKimataifa

Sunak azidi kuongoza mbio kumrithi Johnson

Sunak (kulia) akiwa na Boris Johnson aliyejiuzulu
Spread the love

ALIYEKUWA Waziri wa fedha wa Uingereza, Rishi Sunak ameimarisha nafasi yake ya kuweza kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza, baada ya kuongoza tena katika kura iliyopigwa na wabunge wa chama chake cha Conservative katika mbio za kurithi mikoba ya Boris Johnson aliyejiuzulu.  Inaripoti Mitandao ya kimataifa… (endelea).

Katika kura hiyo iliyopigwa usiku wa kuamkia leo tarehe 19 Julai, 2022, Sunak aliungwa mkono na wabunge 115, akifuatiwa na waziri wa zamani wa ulinzi, Penny Mordaunt aliyechaguliwa na wabunge 82.

Waziri wa mambo ya nje, Liz Truss amekuja katika nafasi ya tatu kwa kupata kura 71, naye Kemi Badenoch alimudu kura 58 na kufanikiwa kubaki katika mchuano huo.

Tom Tugendhat aliambulia kura 31 na hivyo kuenguliwa, na kubakisha watia nia wanne tu katika kinyang’anyiro hicho.

Wawili watakaosalia baada ya duru nyingine ya mtoano bungeni, watapigiwa kura na wanachama wa Conservative na mshindi atakuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!