Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waomba wanahabari wapewe kinga, wawezeshwe kiuchumi
Habari Mchanganyiko

Waomba wanahabari wapewe kinga, wawezeshwe kiuchumi

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania, imeshauriwa kufanya marekebisho ya sheria zinazosimamia tasnia ya habari, yatakayowezesha wadau wake hususan waandishi wa habari,  kuwa huru kutekeleza majukumu yao. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa hivi karibuni, katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kwenye kuandika habari za mahakama na haki za binadamu, iliyoandiliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) na kufanyika mkoani Morogoro.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Albert Msando, alishauri kuwe na utaratibu maalum utakaowawezesha kiuchumi waandishi wa habari, kama wanavyowezeshwa watu wa makundi mbalimbali.

“Asilimia kubwa ya kukosekana kwa uhuru wa habari ni umasikini wa waandishi wa habari, huwezi kuwa huru kama unategemea mtu mwingine. Tubebe hili la uwezeshaji kiuchumi kwa waandishi wa habari, kama ilivyo kwa makundi yote yenye uwezeshaji wa kiuchumi,” alisema Msando na kuongeza:

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jaji Mstaafu Robert Makaramba, alisema marekebisho ya sheria hizo, yatawezesha wanahabari kupata kinga katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Kuna suala la kinga kwa wanahabari, ndiyo maana tasnia inatakiwa iwe professional ili wapate kinga na walindwe kisheria na ndiyo lengo la marekebisho ya sheria,” alisema Jaji Makaramba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!