Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko SUKITA yataka kamati za kutokomeza ukatili zianzishwe nchi nzima
Habari Mchanganyiko

SUKITA yataka kamati za kutokomeza ukatili zianzishwe nchi nzima

Spread the love

SERIKALI imetakiwa kuhakikisha kamati za Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA), ngazi ya kata, zinaundwa nchi nzima ili kulinda haki za wananchi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 27 Julai 2023 katika mjadala kuhusu ujenzi na nguvu za pamoja juu ya kupambana na ukatili wa kijinsia na hamasa ya uundwaji kamati za MTAKUWWA, ulioandaliwa na Shirika la Usawa wa Kijinsia Tanzania (SUKITA) na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa SUKITA, Msafiri Mwajuma Mariam amesema kamati hizo zikiundwa zitasaidia kupata mwarobaini wa matatizo ya ukatili wa kijinsia.

“Tunahamasisha uundwaji wa kamati za MTAKUWWA, kwani kama shirika tunaamini kama kamati hizi zikifanya kazi ipasavyo haya ya ukatili wa kijinsia yatakwisha kabisa,” amesema Msafiri.

Akisoma risala ya shirika hilo mbele ya mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Hilda Malosha, Mwanachama wa SUKITA, Cecilia Kimaro, ameiomba Serikali iendelee kutoa vibali kwa asasi za kiraia kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma juu ya namna ya kutokomeza vitendo hivyo.

Afisa Miradi wa SUKITA, Jamaica Adam, amesema shirika lake limeandaa mjadala huo kwa ajili ya wadau kupata nafasi ya kubadilishana uzoefu wa namna ya kukabiliana na vitendo hivyo.

Akijibu risala ya SUKITA, Malosha amesema halmashauri hiyo itaendelea kutoa vibali kwa asasi za kiraia ili ziendelee kufanya kazi yake ya kutokomeza vitendo vya ukatili kwa ajili ya kuisaidia serikali.

“Elimu ni muhimu, kokote unapokuwa unawajibika kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia ujue unapata swawabu kwa Mungu. Tutafurahi zaidi kama mtakuja kutoa elimu shuleni kote na tunaahidi kama halmashauri tuko pamoja na nyie,” amesema Malosha.

Naye Polisi Kata Makuburi, ASP Omary Fundi, ameishauri jamii iangalie kwa kina tatizo la ukatili wa kijinsia kwa kuwa ili liishe inatakiwa nguvu ya pamoja.


“Ukatili wa kijinsia ni mada pan asana, kwa hiyo ni jambo ambalo linahitaji tuliangalie kwa kina tuone namna gani tutapata suluhu,” amesema ASP Fundi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!