Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu St Mary Goreti yasifiwa kwa mchango wake katika jamii
Elimu

St Mary Goreti yasifiwa kwa mchango wake katika jamii

Spread the love


MBUNGE wa Moshi Mjini, mkoani Kilimanjaro, Priscus Tarimo, ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari ya St Maria Goreti mchangao mkubwa inayotoa katika kukuza sekta ya elimu na mchango wa shule hiyo kwa jamii kwa ujumla Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro  … (endekea),

Tarimo alitoa pongezi hizo wakati wa kambi maalum ya kupima afya na kuchangia damu iliyoandaliwa na uongozi wa shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yanayooendelea ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo.

“Shule hii ilianza kama shule ya sekondari ya kawaida, baadaye ikawa ya hadi kidato cha sita; sasa hivi uongzi wa shule hii umeanzisha shule ya awali pamoja nay a msingi, haya ni mafanikio makubwa kwa shule yenu na mchango mkubwa katika kukuza sekta ya elimu hapa nchini,” alisema.

Aidha aliupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuchangia maboresho ya mazingira mkoani Kilimanjaro kwa kuchangia miche ya miti na uandaji wa miti katiak wilaya zote za Mkoa kama sehemu ya maadhimisho.

“Nimeelezwa ya kuwa mmechangia miti 2,000 itakayopandwa maeneo mbalimbali hapa mkoani Kilimanjaro, huu ni mchango mkubwa katika kuboresha mazingira haswa ikitiliwa maanani ya kuwa moja wapo ya ajenda za serikali ni kuhakikisha mazingira yanaboreshwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi”, alisema.

Kuhusu kambi hiyo, Bw Tarimo alisema pia ni njia nzuri kama sehemu ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 25 ya shule ambapo alisema wananchi watapata fursa ya kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wananchi wengine sambamba na kupima hali zao za afya bure.

Bw Tarimo ambaye katika hafla hiyo alijisajili kama mshiriki wa mbio zilizoandaliwa kama sehemu ya maadhimisho hayo, pia alioupongeza uongozi wa shule hiyo kwa kuandaa mbio hizo ambazo alisema zitachangia kuboresha maisha ya washiriki sambamba na kukuza sekta ya michezo.

Awali akimkaribisha Mbunge huyo kutoa salamu zake, Mkuu wa shule ya sekondari ya St Maria Goreti Sr Clementina Kachweka, alisema kambi hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuchangia damu kwa wahitaji, haswa ikitiliwa maanani mahitaji ya damu yamekuwa ni makubwa katika taasisi za tiba mkoani Kilimanjaro.

“Mbali na kuchangia damu, pia watu watapata fursa za kupima afya zao bure, lengo ni kuwapa watu kuweza kujua hali zao za kiafya na pale anapogundulika kuwa na maradhi aweze kuanza tiba mapema”, alisema.

Aliishukuru hospitali ya KCMC ya Moshi kwa kuwa mstari wa mbele katika kuratibu zoezi hilo la upimaji afya na kuchangia damu huku wakisaidiwa na wataalamu wengine kutoka Hospitali ya St Joseph, Hospitali ya Huruma na Masispaa ya Moshi (kitengo cha Damu Salama). Zaidi ya watu 1000 wakiwemo wanafunzi walipima afya na kupata ushauri mbalimbali na watu 50 walichangia damu itakayookoa maisha ya watu 150.

Sr Clementina aliendelea kusema kuwa mbali na zoezi hilo, pia tayari uongozi wa shule hiyo umeshafanya matukio mengine ikiwemo uzinduzi wa maadhimisho hayo ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa shule hiyo na ugawaji wa miti 2,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambayo itapandwa maeneo mbalimbali mkoani humo.

“Mbali na shughuli hizo, pia zitafuata shughuli zingine ambazo ni pamoja na mbio/matembezi ya hisani km 10 na km 5 zitakayofanyika Agosti 26, 2023 na ambazo usajili wake umeanza leo, (July 7)”, alisema.

Shughuli zote za kuelekea Jubilee ya miaka 25 ya St Mary Goreti zinaratibiwa na kampuni ya Executive Solutions Ltd, Moja makampuni yanayoongoza nchibi katika kuratibu matukio na masuala ya habari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

error: Content is protected !!