Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika aipa maagizo Serikali sakata la wafugaji Ngorongoro
Habari za Siasa

Spika aipa maagizo Serikali sakata la wafugaji Ngorongoro

Spika Dk. Tulia Ackson
Spread the love

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameitaka Serikali kushughulikia sakata la wafugaji wilayani Ngorongoro kuuziwa mifugo yao zaidi ya 1,000 kinyume cha sheria, kisha ipeleka bungeni jijini Dodoma, ripoti juu ya suala hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Spika Tulia ametoa agizo hilo leo tarehe 9 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma, baada ya Mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangay, kuomba ufafanuzi wa Serikali juu ya sakata hilo linalodaiwa kuanza tarehe 26 Oktoba mwaka huu.

“Hili suala nimelikabidhi kwa Serikali ili iweze kulitazama hili jambo vizuri. Tuipe muda serikali tuweze kujielekeza vizuri, sababu mbunge alisema mahakama imetoa amri bila wananchi kusikilizwa, sasa jambo hili limeamuliwa na mahakama hivyo wanatakiwa kwenda mahakama ya juu,” amesema Spika Tulia.

Agizo hilo la Bunge, limekuja siku moja baada ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) 16, zikiongozwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), kuutaka mhimili huo kuingilia kati ili wafugaji wapatiwe haki zao.

Awali, Waziri wa Maliasili na Utalii, Anjellah Kairuki, akitoa ufafanuzi wa suala hilo, alisema mifugo hiyo imepigwa mnada kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma, katika kesi ya jinai Na. 10/2023, iliyofunguliwa kwa shtaka la mifugo kuingia hifadhini kinyume cha sheria.

Kairuki alisema mifugo inayodaiwa kupigwa mnada ni ng’ombe 806, kondoo 420 na mbuzi 100, ambao inadaiwa kupigwa mnada kwa gharama ya Sh. 169 milioni.

Sakata hilo linadaiwa kuibuka baada ya baadhi ya maofisa wa uhifadhi Ngorongoro, kudaiwa kuswaga mifugo hiyo kutoka vijijini kwenda hifadhini kwa makusudi, lengo likitajwa kuwatengenezea kesi wafugaji ili kuitafisha kwa makusudi.

Ole Shangai alidai kuwa, baadhi ya maofisa wa Hifadhi ya Ngorongoro, walifanya hujuma kwa kutengeneza kesi iliyodai kuwa mifugo iliyokamatwa hifadhini kinyume cha sheria, haikuwa na mmiliki na kuiomba mahakama itoe kibali ipigwe mnada, ilhali wakijua kwamba wamiliki wa mifugo hiyo wapo.

Mbunge huyo anadai kuwa, alipopata taarifa kwamba kesi hiyo imefunguliwa alifanya jitihada za kuzungumza na Mamalaka ya Hifadhi Tanzania (TANAPA), ili kuwajuza kuwa mifugo hiyo ina wamiliki wake hivyo wako tayari kulipa faini kama itabainika wana makosa, lakini bado ilipigwa mnada kwa kigezo kuwa haina wenyewe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!