Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Mawakili 10 TLS kumtetea mjane aliyehukumiwa miaka 22 kwa kuuza nyama ya swala
Habari Mchanganyiko

Mawakili 10 TLS kumtetea mjane aliyehukumiwa miaka 22 kwa kuuza nyama ya swala

Spread the love

CHAMA cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) Kanda ya Iringa kimewataja mawakili 10 waliopangwa katika maandalizi na usikilizwaji wa rufaa ya hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi namba 28 ya mwaka 2022 inayomuhusu mjane Maria Emirio Ngoda aliyehukumiwa miaka 22 kwa kosa la kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala. Anaripoti Mwandishi Wetun …(endelea).

Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Mkoa wa Iringa tarehe 3 Novemba 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa, Said Mkasiwa aliyedai kuridhishwa pasipo shaka kuwa mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000.

Akitoa taarifa ya mchakato wa rufaa hiyo ikiwa ni siku moja baada ya TLS kanda hiyo kutangaza kumsaidia mjane huyo kufanya utetezi huo bure, Mwenyekiti wa TLS kanda ya Iringa, Wakili Moses Ambindwile alisema;

“TLS kwa kupitia mawakili hao tayari imepeleka Mahakama Kuu Kanda ya Iringa taarifa ya kukata rufaa na sasa tunasubiri kumbukumbu namba ya mfumo ili taratibu zingine ziendelee.

Mbali na yeye Wakili Ambindwile aliwataja mawakili wengine watakaosimama kumtetea mjane huyo ambaye rufaa ni sehemu ya haki yake kuwa ni pamoja na Dk Rwezaula Kaijage, Frank Ngafumika, Barnabas Nyalusi, Jane Massey, Samson Rutebuka, Joshua Chusi, Innocent Kibadu na Cosmas Kishamawe.

Tangu uhukumu hiyo dhidi ya mjane huyo itolewe na kuripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kumejitokeza mijadala na hisia tofauti kuhusu maamuzi hayo ya Mahakama.

Baada ya TLS kujitokeza kumsaidia mjane huyo, jana imeripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu nia ya Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsaidia mjane huyo kukata rufaa.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda imeonesha kwamba “Pamoja na kwamba maamuzi ya mahakama ni maamuzi ya mahakama” UWT inajitolea kumsaidia mjane huyo katika rufaa yake kwa kuhakikisha anapata uwakilishi wa mawakili wa kutosha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!