Monday , 11 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Vodacom yagawa Bima kwa watoto 1,000 bure
Habari Mchanganyiko

Vodacom yagawa Bima kwa watoto 1,000 bure

Spread the love

 

KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua kampeni ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’ itakayotoa Bima ya Afya kwa watoto 1,000 watakaozaliwa ndani ya kupindi cha siku 70 ambayo kampeni hiyo itakuwa inaendeshwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kampeni hiyo imezinduliwa leo tarehe 9 Novemba 2023 itadumu kwa muda wa miezi mitatu na siku 10 yaani wiki 10 sawa na siku 70.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Linda Riwa, Mkurugenzi wa Biashara na Masoko amesema kuwa kampuni hiyo itatoa bima kubwa za afya kwa watoto 1,000 watakaozaliwa katika kipindi hiki.

“Mwaka huu tumeleta kitu cha tofauti kipindi hiki cha sikukuu watu wanajumuika kwa hiyo msimu huu tunakwenda kugusa maisha ya zaidi ya watoto 1,000 watakaozaliwa msimu huu watoto hao na wazazi wao watapewa bima kubwa ya Afya ya mwaka mzima kutokana Voda,” amesema Riwa.

Riwa amesema kuwa bima hiyo itawezesha kupata huduma zote za afya ndio maana tumesema bima kubwa. Utaratibu wa kuwafikia watoto hao kampuni hiyo itawasiliana na maofisa afya wa mikoa yote nchini.

Mbali kuigusa jamii kwa kutoa bima kampuni hiyo itawapa wateja wake zawadi mbalimbali .

“Wateja watajishindia zawadi mbalimbali kuanzia mil10 na , Pikipiki Smart TV , Smart Phone, Router ya Internet kila siku wateja wetu watashinda zawadi.

“Ili ushindi uwe na line ya Vodacom pia kutumia Mpesa mara kwa mara na pia kutumia vifurushi vya kawaida vya kila siku sambamba na kutumia MPesa App , na Vodacom app”

Kwa upande wake Nguvu Kamando, Mkurugenzi wa Huduma za kidigitali amesema kuwa kampani hiyo itawaburudisha na kuwapa zawadi wateja wake kupitia kampeni ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’.

“Sio tu kwenye mawasiliano hata kwenye burudani vodacom tuko mbele…tumewaletea App ya Mdundo ambayo ukidownloada utapata mix kali za muziki kutoka kwa ma Dj wakali utazipata bila matangazo yoyote,” amesema Kamando.

Amesema kupakua na kusikiliza muziki kwenye app ya Mdundo unaingia kwenye Kinyang’anyiro cha kushinda pesa na zawadi mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Kesi ya mfanyakazi wa CRDB itaendelea J’tatu

Spread the love  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam inatarajia...

Habari Mchanganyiko

Mawasiliano Dar – Bagamoyo yarejea

Spread the loveMAWASILIANO ya barabara ya Mkoa wa Pwani na Dar es...

Habari Mchanganyiko

Tanesco: Mvua chanzo kukatika umeme leo

Spread the loveShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limedai kuwa hitilafu iliyojitokeza katika...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Zara tours yajivunia kupandisha wageni 228 Mlima Kilimanjaro

Spread the loveKampuni ya utalii ya Zara tours ya mjini Moshi mkoani...

error: Content is protected !!