Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari Simba yaomba kupewa ulinzi Afrika Kusini
Habari

Simba yaomba kupewa ulinzi Afrika Kusini

Spread the love

 

KLABU ya Soka ya Simba imeziomba mamlaka husika kuwapatia ulinzi wa kutosha wakati wa safari yao kuelekea nchini Afrika Kusini kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Orlando Pirates kufuatia kuonekana kwa dalili za uvunjifu wa Amani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa marudiano wa robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, utapigwa Soweto Afrika kusini tarehe 24 2022.

Simba imedhamilia kupeleka maombi kwa serikali ya Tanzania sambamba na serikali ya Afrika Kusini kupatia ulinzi huo kufuatia kauli za chuki zilizotolewa na kocha msaidi wa klabu ya Orlando Pirates Mandla Ncikazi Kwa kudai kuwa wamefanyiwa vitendo visivyokuwa vya kiungwana na Simba.

Ncikazi alitoa malalamiko hayo mkwenye mkutano na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kumalizika kwenye dimba la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, ambapo Simba walifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0.

Katika malalamiko yake, Ncikazi alilalamikia suala la mwamuzi kuwapa penati Simba, katika tukio ambalo anaamini lilikuwa na utata bila kwenda kutazama kwenye VAR, mabyo ilitumika kwenye maamuzi sehemu ya mchezo huo.

Aidha kocha huyo msaidizi alitoa kauli za kuonesha kwamba wamefanyiwa vitendo visivyo vya kiungwana nje ya uwanja bila kuvielezea ni vya aina gani kabla ya mchezo huo.

Kwa mantiki hiyo klabu ya Simba sambamba na kutaka ulinzi lakini pia imedhamilia kufikisha barua rasmi ya malalamiko kwenye shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kuhusu kauli zilizotolewa na kocha huyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!