Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba SC. wamtimua kocha mkuu Zoran Maki
MichezoTangulizi

Simba SC. wamtimua kocha mkuu Zoran Maki

Spread the love

KLABU ya Soka ya Simba SC. imemtimua Kocha Mkuu wa kikosi cha timu hiyo, Zoran Maki baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja  mkataba. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo … (endelea).

Pia imefikia makubaliano ya kusitisha mikataba ya Kocha wa viungo, Sbai Karim na Kocha wa Makipa  Mohamed Rachid.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 6 Septemba, 2022 na Afisa mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Barbara Gonzalez imeeleza kuwa uongozi wa klabu hiyo unawashukuru makocha hao kwa mchango wao ndani ya klabu yetu na inawatakia kila heri katika majukumu yao mapya.

“Kuelekea mchezo wetu wa kesho dhidi ya KMC kikosi chetu kitakuwa chini ya Kocha msaidizi, Selemani Matola.

“Tayari mchakato wa haraka wa kutafuta makocha wapya umeanza na unatarajiwa kukamilika hivi punde,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari MchanganyikoTangulizi

Walimu 5000 Songwe waililia CWT kuwanyima sare

Spread the loveZaidi ya walimu 5000 ambao ni wanachama wa Chama cha...

error: Content is protected !!