Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Shule ya East Africa yaahidi kufanya maajabu kitaaluma
Elimu

Shule ya East Africa yaahidi kufanya maajabu kitaaluma

Spread the love

MWENYEKITI wa Wazazi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Dk. Rose Rwakatare, ameishukuru serikali kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Alitoa shukrani hizo jana jijini Dodoma wakati wa mahafali ya kwanza ya darasa la saba shule ya Awali na Msingi ya East Africa ya mkoani Dodoma.

“Serikali ilipohamia hapa wakati wa hayati Rais Magufuli alitoa wito kwa wawekezaji kuwekeza miundombinu mbalimbali ili kusaidia kutoa elimu na sisi kama watua mabo tumebobea katika elimu tuliamua kuwekeza kwa kujenga shule hii ili kuweza kutoa elimu bora”alisema

Alisema lengo la shule ni kuunga mkono jitihada za serikali katika utoaji wa elimu bora kwa watoto wa kitanzania ili kuwawezesha kutoa ushindani katika soko la ajira duniani.

Alisema shule hiyo itaendelea kuwa shule bora kwa kuhakikisha inakuwa kwenye orodha za kuu kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa na kimkoa .

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, alisema kutokana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili  wazazi wanatakiwa kuwalinda watoto ili wasiharibiwe na tamaduni za kigeni ikiwemo kujihusisha na vitendo vya ndoa za jinsia moja.

Mbaga, alisema hivi sasa Dunia imeharibika sana hivyo wazazi wanao wajibu wa kuhakikisha wanawalinda watoto wao ili wasiharibiwe na tamaduni za mataifa mengine.

“Hivi sasa ndugu zangu dunia imeharibika sana vitendo vya mmomonyoko wa maadili vimekithiri sana hivyo wazazi mnapaswa kuwalinda watoto ili wasiharibiwe na tamaduni za mataifa mengi.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa shule ya awali na msingi East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma mwishoni mwa wiki

“Mataifa ambayo yamekuwa yakihamasisha masuala ya ndoa za jinsia moja na mambo mengine ambayo ni kunyume ya tamaduni za kitanzania na nikinyume na mpango wa Mungu”alisema Mbaga

Aidha, aliwataka wazazi kuacha tabia ya kutelekeza suala la malezi ya watoto kwa walimu pekee yao bali wanapaswa kuwasimamia na kuwafuatilia kila wakati ili wabaini vikwazo ambayo wanakabiliwa navyo.

“Wazazi hatupaswi kuacha suala la malezi kwa walimu pekee yao bali tuhakikishe kuwa tunawafuatilia watoto wetu kwa kushirikiana na walimu ili kuwasaidia wasiingie kwenye mikono ya shetani hali ibadilika sana hivi sasa watoto wamekuwa na tabia za ajabu ambazo kama hatutakuwa makini nao tutawapoteza”alisema

Kadhalika, aliwataka walimu kuhakikisha kuwa wanasimamia watoto hasa wanapokuwa katika mabweni ili kubaini kama kuna mabadiliko yoyote ya kitabia na kuchukua hatua mapema kabla ya kundi kubwa kuharibiwa.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa shule ya awali na msingi East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma mwishoni mwa wiki

Vile vile, aliipongeza shule hiyo kwa kuunga mkono wa jitihada za serika katika uwekezaji kwenye sekta ya elimu ili kutoa elimu bora kwa watoto wa Kitanzania.

“Mkurugenzi niwapongeze sana kwa uwekezaji huu katika sekta ya elimu sisi chama pamoja na serikali kwa ujumla tutaendelea kutoa ushirikinao kwenu ili mfikie malengo yenu”alisema

Alisema azma ya serikali ya awamu ya sita ni kuboresha elimu ambapo hivi sasa imefanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa madarasa,maabara, mabweni pamoja na miundombinu mingine ili kuinua kiwango cha elimu nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

error: Content is protected !!