VIJANA wametakiwa kushirikiana katika kuleta uhuru wa kiuchumi, ili kuondoa changamoto ya ugumu wa maisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Wito huo imetolewa hivi karibuni na Naibu Msemaji wa Vijana, Kazi na Ajira, wa Chama cha ACT-Wazalendo, Felix Kamugisha, katika ziara yake aliyofanya kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Kamugisha alisema vijana wa zamani wakiongozwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, walipambana kuleta uhuru wa kujitawala, hivyo vijana wa Sasa wanapaswa kupigania uhuru wa uchumi na kuchagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kulinda maslahi Yao.
“Sisi vijana tunatakiwa kufanya mabadiliko ya nchi yetu, waliopigania uhuru walikuwa vijana mpaka leo tuko huru lakini hatuko huru kiuchumi, kuchagua wawakilishi Wetu bungeni,” alisema Kamugisha.
Kamugisha alisema “matatizo hata tuliyokuwa nayo sio bahati mbaya, wala hayakutoka kwa Mungu, yanasababishwa na watu tuliowapa dhamana ya kutuongoza. Badala ya kulinda maslahi yetu lakini wanakwenda bungeni kupanga ambayo hatujawatuma sisi.”
Msemaji huyo wa Vijana ACT-Wazalendo, alisema kundi hilo linapaswa kuhakikisha linajitokeza kushiriki katika chaguzi mbalimbali, ili kuchagua viongozi wazalendo watakaotumia rasilimali za nchi kuleta maendeleo na kutatua changamoto zao, ikiwemo ukosefu wa Ajira.
Leave a comment