Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Sheria ya kudhibiti maandamano yaandaliwa kumfunga Odinga ‘speed governor’
Kimataifa

Sheria ya kudhibiti maandamano yaandaliwa kumfunga Odinga ‘speed governor’

Spread the love

WIZARA ya mambo ya ndani ya Kenya inapendekeza mabadiliko ya sheria za usalama ambayo yatafanya iwe vigumu kwa watu kufanya maandamano. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Katiba ya nchi hiyo inawapa Wakenya haki ya kukusanyika, kuandamana na kulalamiki madhila, lakini washiriki lazima wawe watulivu na bila silaha.

Maandamano yaliyofanyika wiki iliyopita katika ngome za upinzani yalisababisha kifo cha mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya watu wengi.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya

Akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu mapendekezo hayo, Waziri wa Mambo ya ndani ya Kenya, Kithure Kindiki amesema mabadiliko yaliyopendekezwa na wizara yanalenga kupunguza idadi ya watu wanaofanya maandamano wakati wowote na kuwafanya waandamanaji kulipa gharama za kusafisha maeneo ya maandamano yao.

Waandamanaji lazima pia waombe ridhaa kutoka kwa watu walioathiriwa na maandamano hayo. Waandamanaji pia watawajibika kulipa fidia kwa wale walioathiriwa na shughuli zao.

Katika mapendekezo ya mabadiliko hayo, wizara ya mambo ya ndani pia inataka kutengwa kwa maeneo ambayo watu wanaweza kukusanyika na kufanya maandamano.

“Haiwezekani kwa vyombo vya usalama kuruhusu umati wa watu kuzurura mitaani na vitongoji wanavyopenda wakiwa wamebeba mawe na silaha nyingine za kukera huku wakiimba nyimbo za kisiasa na kutatiza shughuli za kila siku za wengine,” ilisema taarifa ya wizara hiyo..

Mabadiliko yaliyopendekezwa yamekosolewa na baadhi ya watu na kuona kama dharau kwa misingi ya jamii iliyo wazi na kidemokrasia na kama kwamba sheria inayokiuka katiba.

Haya yanajiri huku upande wa upinzani ukiapa kuendelea na maandamano dhidi ya gharama ya juu ya maisha na madai ya udanganyifu katika uchaguzi mkuu uliopita.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!