Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima
Kimataifa

Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima

Spread the love

MSAFARA wa kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga umepita katika eneo la Kawangware jijini Nairobi nchini Kenya na kupata fursa ya kuwahutubia wakazi hao lakini baada ya muda mfupi, wafuasi wake wakatimuliwa kwa mabomu ya machozi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

“Sisi wana-Azimio tunasema gharama ya maisha zishuke, bei ya unga irudi chini, bei ya mafuta irudi chini, sukari irudi chini na ‘server’ ifunguliwe,” amesema Raila kwenye msafara huo.

Viongozi walioandamana na Raila ni Martha Karua, Eugene Wamalwa, Wycliffe Oparanya, Jeremiah Kioni na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha Roots Party George Wajackoyah na miongoni mwa viongozi wengine.

Wakati akiendelea na maandamano hay oleo tarehe 27 Machi 2023, Odinga dakika chache baada ya kuanzisha maandamno hayo huku msafara wa kiongozi huyo ukipenya katika makazi hayo, maofisa wa polisi waliwarushia mabomu ya machozi waandamanaji waliokuwa wamebeba matawi ya miti, mabango, sufuria na baadhi ya vyakula ili kupinga hali ya juu ya maisha.

Hatua hiyo inajiri baada ya Inspekta mkuu wa Polisi IGP nchini humo, kudai kwamba maandamano hayo yalikuwa haramu.

Haya yanajiri huku genge la vijana likivamia shamba la Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta lililoko Eastern Bypass. Dhamira ya watu hao haijabainika kufikia sasa.

Kenyatta alimuunga mkono Raila kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 9 Agosti 2022.

Serikali ya Kenya inayoongozwa na Rais William Ruto inalaumiwa kwa kile upinzani inachodai kuwa ni kuwanyanyasa raia kwa kusababisha ongezeko la gharama za maisha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!