Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yasikia kilio changamoto hedhi salama, yatoa ahadi
Habari Mchanganyiko

Serikali yasikia kilio changamoto hedhi salama, yatoa ahadi

Spread the love

SERIKALI imesema inafanyia kazi maombi ya wadau kuhusu uboreshaji mazingira ya hedhi salama kwa watoto wa kike. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Ahadi hiyo imetolewa leo tarehe 30 Julai 2023 na Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Angellah Kairuki, akizungumza katika mbio za “Run For Binti Marathon” zilizoandaliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF) na Smile for Children (S4C), jijini Dar es Salaam.

Ni baada ya wadau hao kuomba Serikali iondoe au ipunguze kodi katika taulo za kike (sodo), ili kushusha bei, pamoja na kuboresha miundombinu ya vyoo vya shule kwa kujenga vyumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kubadilisha sodo wakiwa katika kipindi cha hedhi.


“Kuhusu punguzo la kodi tutaenda kuwasilisha katika Wizara ya fedha, ili waweza kuangalia wanapokuja na sheria ya muswada wa  fedha mwaka kesho, wakilifanyie kazi. Lakini ikifika Novemba kuna kikosi kazi maalum cha kupitia Kodi, mtaalikwa kushiriki ili mjenge hoja iweze kueleweka,” amesema Kairuki.

Aidha, Kairuki amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya shule nchini, ili kujenga vyumba maalum kwa ajili ya wanafunzi wa kike kubadilisha sodo, ambapo kwa sasa imeshajenga katika shule 1,283, huku ikitarajia kufikia shule 2,500 ifikapo 2026.

Kairuki ametaka fedha na vitu vilivyokusanywa katika mbio hizo, zifikie walengwa kwa ajili ya kuwasaidia, hasa wasichana wasiokuwa na uwezo.

“Serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan, imekuwa ikijenga shule nyingi kwa fedha za Serikali na wadau wa maendeleo wameendelea kuwa sehemu kubwa ya mafanikio haya, tunaamini mbio hizi zitasaidis kimstiri mtoto wa kike kuongeza kujiamini hata atakapokuwa hedhini bila kuathiri masomo yake,” amesema Kairuki.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala,  alisema fedha zinazoendelea kukusanya kupitia mbio hizo, zitatumika kujenga miundombinu ya vyoo itakayowezesha wasichana kujistiri wakati wa hedhi, kugawa sodo zinazotumika zaidi ya mara Moja.


Pamoja na kutoa fedha kwa vikundi vya kina mama wajasiriamali ili waweze kutengeneza sodo nyingi, pamoja na kuwaongezea kipato.

Amesema wanufaika wa fedha hizo ni wanafunzi zaidi ya 15,000, na vikundi viwili vya wajasiriamali kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.

Naye Mkurugenzi wa S4C, Flora Njelekela, alisema “kwa pamoja twende kuzitatua changamoto hizi na hili ndilo lengo la S4C na LSF, utufikishie salamu kwa Rais Samia kwamba sisi wadau tungependa kuona kampeni hii inafikia mbali zaidi.”

“Na pia kama tutaweza kuondolewa kodi ya ongezeko la thamani kwa sodo au kupunguzaa, itasaidia sana kupunguza gharama zake na kuongeza mapato ya Serikali,” amesema Flora.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!