Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Raila, Ruto sasa kupatanishwa na Obasanjo
KimataifaTangulizi

Raila, Ruto sasa kupatanishwa na Obasanjo

Spread the love

RAIS mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo ataongoza kamati ya watu 10 katika mazungumzo kati ya Rais wa Kenya, William Ruto na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Hayo yalitangazwa jana Jumamosi, tarehe 29 Julai, kupitia tamko la pamoja la muungano wa Azimio la Umoja na Kenya Kwanza.

Kwa mujibu wa tamko hilo, kila upande utatoa watu watano kuingia katika timu ya majadiliano.

“’Sisi uongozi wa muungano wa Azimio la Umoja tumeshauriana na muungano wa Kenya Kwanza chini ya uongozi wa Mheshimiwa Olusegun Obasanjo kuhusu hali ya taifa letu, tumedhamiria kutatua tofauti zetu kwa amani kwa manufaa ya watu wetu wote,’’ taarifa hiyo ilisema.

‘’Mawasiliano zaidi ya mpango huu, yatawasilishwa kwa wakati ufaao,’’ taarifa hiyo ilieleza.

Makubaliano ya viongozi hao wawili kuunda kamati, pengine huenda ni ishara kwamba wanakaribia kufikia makubaliano kutatua mgogoro wa kisiasa ambao umekumba taifa la Kenya kutokana na maandamano ya hivi karibuni ambayo yamekuwa yakiandaliwa na muungano wa upinzani kupinga kuongezeka kwa gharama ya maisha.

Jumanne iliyopita, Ruto alisema yuko tayari kukutana ana kwa ana kufanya mazungumzo na Raila na wakati wowote.

Akizungumza na wanahabari wa Kimataifa wiki iliyopita, Raila aliishutumu serikali ya Ruto kwa kukatiza juhudi za upatanishi za Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Raila alifichua kuwa Rais Samia alizuru Kenya majuma kadhaa yaliyopita, lakini hakuna mawasiliano ambayo serikali ilifanya naye kuhusu jitihada za kuwaleta pamoja Ruto na Odinga.

Chanzo cha uhakika kutoka serikali ya Tanzania ambacho hakikutaka kutajwa jina lake, kiliithibitishia BBC Swahili kwamba madai ya Raila yana ukweli.

Hata hivyo, akizungumza na wanahabari msemaji wa Ikulu ya Kenya, Hussein Mohammed alipuuza madai kwamba Ruto alikataa kukutana na Samia akidai kuwa itifaki haikuzingatiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

error: Content is protected !!