Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu
Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Furaha Domic
Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu wawili akiwamo mpwa wa hayati John Magufuli, Furaha Dominic kwa tuhuma za kuratibu mtandao wa uhalifu wa kusambaza picha za ngono kwa lengo la kujipatia pesa. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Akizungumza na waandishi wa Habari jana Jumatatu jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum- SACP Jumanne Muliro amesema watu hao walikuwa wakisambaza picha hizo huku wakiwatisha wahusika ili kujipatia fedha.

Aliwataja watu hao ni; ”Furaha Dominic Jacob (32) mkazi wa Masaki na Mustapha Kihenge (28) Mkazi wa Mwenge TRA, wanatuhumiwa kutenda makosa ya uhalifu wa kimtandao. Wanadaiwa kusamba picha chafu za video za watu sizizo na maadili kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia za vitisho.

“Watuhumiwa wote wawili watafikishwa mahakamani leo  Jumanne ili kukabiliana na tuhuma hizi,” alisema Muliro.

Furaha Dominic Jacob ambaye alikuwa mmoja wa makada wa CCM waliokuwa wameomba ridhaa ya chama hicho katika mbio za ubunge – Kawe kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, alishinda kura za maoni lakini akaenguliwa na Rais Magufuli ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM.

Furaha alishinda kura za maoni ndani ya CCM kwa kupata  kura 101, Angela Kizigha alipata kura 85, Askofu Josephat Gwajima kura 79, Benjamin Sitta kura 61 na Vicent Mashinji ambae alihama CHADEMA na kwenda CCM aliibuka na kura 2.

Mwaka juzi Furaha alihojiwa na kituo cha runinga cha Star Tv na alielezea namna hayati Magufuli alivyokuwa amezungukwa na watu aliodai ni waongo, wazushi na wafitini (kupe) waliosababisha wakati mwingine afanye maamuzi yasiyo sahihi yaliyoumiza wasio na hatia.

Alidai watu hao walimuwekea zengwe hadi akaukosa ubunge wa Kawe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!