Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali, wadau watakiwa kulinda viumbehai
Habari Mchanganyiko

Serikali, wadau watakiwa kulinda viumbehai

Spread the love

SERIKALI, wadau kutoka sekta binasi, vyombo vya habari na jamii wameshauriwa kushirikiana kuhifadhi, kutunza mazingira na wanyamapori ili vizazi vijavyo viweze kurithi na kufaidika na rasilimali hizo ambazo zinaanza kutoweka. Anaripoti Selemani Msuya … (endelea).

Ushauri huo umetolewa na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC), Dk. Abdallah Katunzi wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Waandishi hao ni wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (JET) ambao walishiriki mafunzo ya siku mbili yaliyofadhiwa na Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili.

Dk. Katunzi amesema kumekuwepo na kasi kubwa ya uharibifu wa uhifadhi, mazingira na ujangili wa wanyamapori ambao wamekuwa na mchango mkubwa kiuchumi na kijamii, hivyo ni lazima kuwepo juhudi za pamoja za kukabiliana na hali hiyo.

“Hifadhi na wanyamapori vinapaswa kulindwa na kizazi cha sasa, ili watoto na wajukuu zetu waweze kuvikuta na kuweza kutumia. Katika kufanikisha hili vyombo vya habari vinawajibu wa kutengeneza ajenda maalum ambayo itachangia jamii ielewe na kuamini,” amesema.

Mkufunzi huyo amesema asasi za kiraia kama USAID Tuhifadhi Maliasili na JET wameonesha mfano katika kuzilinda na kuzielezea rasilimali hizi, hivyo vyombo vya habari vinawajibu wa kuwa na ajenda maalum na kuisimamia kwa umoja wao, ili iweze kufanikiwa.

Dk. Katunzi amesema eneo hilo likipewa msukumo litaweza kuchangia mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na mazingira, hivyo ni vema waandishi wakaweka mkazo.

“Napenda kuwashauri waandishi wa habari kubobea katika uandishi wa habari za uhifadhi, mazingira na wanyamapori, kwani ni eneo muhimu katika uendelevu wa nchi, lakini pia hata ujangili utadhibitika,” amesema.

Amesema waandishi wa habari wanawake wana nafasi kubwa ya kusaidia eneo hilo kwani madhara ya uharibifu wa mazingira, uhifadhi na wanyamapori kwa asilimia kubwa yanawagusa wao.

Mhadhiri iwapo habari za uharibifu mazingira na ujangili kwa wanyamapori hazitaandikwa kwa usahihi ni wazi kuwa madhara yake yatakuwa makubwa zaidi siku chache zijazo.

Aidha, Dk. Katunzi amewataka waandishi kuandika habari ambazo zinatoa suluhisho, ili kuhakikisha wanakuwa na mchango chanya kwa jamii

Kwa upande wake Meneja Ushirikishwaji wa Sekta Binafsi Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Dk. Elikana Kalumanga amesema ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori umekuwa na matokeo chanya kwa jamii husika, hivyo unapaswa kuepewa kipaumbele.

Dk. Kalumanga amesema kupitia miradi ya kuelimisha, jamii imetambua faida ya maeneo ya hifadhi, hivyo kunufaika na fursa mbalimbali kama kilimo, biashara, ufugaji wa kisasa na kuaminika.

“Sisi kupitia Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili tumeona fursa kama biashara, uhifadhi, kilimo, ufugaji wa nyuki na jamii husika kuaminika katika taasisi za kifedha jambo ambalo awali halikuwepo,” amesema.

Dk. Kalumanga amesema maeneo ya hifadhi yana faida katika kulinda vyanzo vya maji ambayo yanatumika kwa jamii yote, hivyo hakuna njia mbadala katika hilo tofauti na kuhakikisha uhifadhi unaongezeka.

“Uhifadhi una faida nyingi ikiwemo viumbepori, maji, hali ya hewa nzuri na mengine, hivyo hakuna namna ambayo unaweza kufanya uhifadhi bila kushirikisha wadau wote wakiwemo sekta binafsi,” amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Media Foundation (TMF), Dastan Kamanzi amewashauri waandishi wa kuandika habari za uhifadhi na mazingira kwa kuzingatia katiba, sera, sheria, kanuni, miongozo, mipango na mikakati iliypo.

“Ibara ya 14, 27 (1) (2) NA 9 (c) ya Katiba ya Tanzania, sera ya mazingira, sheria, kanuni, mipango na miongozo mbalimbali inaelekeza umuhimu wa kila mtu kushiriki kuhifadhi na kulinda rasimimali misitu na wanyamapori, hivyo hili sio jukumu la mtu mmoja lazima wote tushiriki,” amesema.

Kamanzi amesema waandishi wanawajibu wa kuzingatia sifa muhimu za uandishi ambazo ni uchunguzi, uchambuzi, ushawishi na ujasiri, hali ambayo itawezesha kupatikana maudhui ya kuelimisha, matokeo na uwajibikaji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

error: Content is protected !!