Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Askari wanyamapori 150 kuongeza ufanisi utatuzi migogoro ya kiuhifadhi
Habari Mchanganyiko

Askari wanyamapori 150 kuongeza ufanisi utatuzi migogoro ya kiuhifadhi

Spread the love

 

WIZARA ya Maliasili na Utalii inamatarajio makubwa ya kuimarika kwa shughuli za doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu na hivyo kupunguza migongano baina ya binadamu na wanyamapori baada ya wahitimu zaidi ya kuhitimu fanyi ya uwaskari wa Wanyamapori. Anaripoti Yusuph Kayanda, Ruvuma … (endelea).

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamisha wa Polisi (CP) Benedict Wakulyamba alipokuwa akifunga mafunzo maalum kwa Askari Wahifadhi toka TAWA na kozi Na. 73/2024 kwa Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) katika Chuo cha Likuyu Sekamaganga Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma.

CP Wakulyamba ametaja matarajio mengine ya Wizara kwa wahitimu hao ni Pamoja na kuongezeka kwa ufanisi wa kuitikia kwa haraka kwenye matukio kutokana na kuwa, VGS mnaohitimu mtakuwa kwenye maeneo yenye changamoto na hivyo kuwa mstari wa mbele katika kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu kabla hawajasababisha Mathara.

Aidha CP. Wakulyamba ametoa wito kwa wananchi kuzingatia maelekezo yanayaotolewa na wataalamu wa taasisi za uhifadhi ili kuepuka madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu, kuzingatia mpango wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yaliyopo jirani na hifadhi, mapito na mtawanyiko wa wanyamapori na kujiepusha na tabia ya kupiga wanyamapori wakali kwa kutumia silaha mbalimbali za kimila/jadi pindi wanapoingia kwenye maeneo ya wananchini.

Akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa cha Uhifadhi wa Vijiji kwa Jamii Likuyu Sekamaganga, Jane Nyau ameeleza jumla ya Askari Wahifadhi ishirini na nane (28) toka kwenye Mapori ya Akiba ya Selous na Liparamba na VGS mia moja ishirini na mbili (122) kutoka Wilaya thelathini na nne (34) wamehudhuria mafunzo haya.

Naye Mkurugenzi wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo Dk. Edward Kohi amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia vyuo vyake vya mafunzo itaendelea kutoa Mafunzo mbalimbali ya Uhifadhi kwa kuwajengea uwezo Askari wa Jeshi la Uhifadhi pamoja na Askari wa Wanyamapori wa Vijiji ili kuimarisha Shughuli za Uhifadhi kwa kushirikiana na wanavijiji waishio jirani na Hifadhi.

Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Frankfurt Zoological Society Bi. Kathryn Doody licha ya kuipongeza Serikali kwa kuendesha Mafunzo kwa askari wa Jeshi la Uhifadhi na VGS, amewakumbusha askari hao kutambua kuwa kazi wanayofanya ni muhimu sana, siyo kwa Tanzania tu bali kwa ulimwengu wote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!