Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8
Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Spread the love

 

SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya wilaya ya Moshi inayojengwa katika Kata ya Mabogini ukanda wa tambarare na kuhudumia wananchi zaidi ya 535,803 kutoka majimbo ya Moshi Vijijini na Vunjo. Anaripoti Safina Sarwatt, Kilimanjaro … (endelea).

Hayo yamebainishwa katika tarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi, Shadrack Mhagama aliyoitoa kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za serikali za mitaa iliyotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Hospital hiyo jana Ijumaa.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo ,hadi sasa ujenzi huo unatekelezwa kwenye majengo manne likiwamo jengo la utawala, jengo la mionzi, jengo la kufulia pamoja na jengo la kutolea dawa ambako kiasi cha Sh 800 milioni kitatumika kukamilisha ujenzi huo.

Alisema jengo la utawala limetengewa Sh 407 milioni, jengo la mionzi limetengewa Sh 168 milioni wakati jengo la kufulia likitengewa Sh 135 milioni na jengo la kutolea dawa likitengewa Sh 173 milioni huku akiainisha changamoto za kuchelewa kuanza kwa ujenzi huo kuwa ni mfumo pamoja na mvua.

Mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Hai, Saasisha Mafuwe alitolea ufafanuzi wa sintofahamu ya kujengwa kwa Hospital hiyo eneo la Mabogini kwamba ilitokana na ushauri wa kitaalamu na si kwamba kuna upendeleo.

Kata ya Mabogini ipo kwenye JImbo la Moshi Vijijini ambako mbunge wake ni Profesa Patrick Ndakidemi na Saasisha aliwaeleza wananchi wa jimbo hilo kuwa hakuna ubaguzi wowote uliofanyika kupeleka mradi huo ukanda huo.

“Ndakidemi ni mbunge wa kata zote, ni mbunge wa vijiji vyote na eneo hili ndiyo lilikuwa eneo rafiki kujengwa hapa na siyo kwa sababu anawapenda wale na anawachukia wale hapana, sababu za kitaalamu zinaonyesha ni hapa na serikali imeamua ni hapa na watu wa mabogini ni watu lazima kituo kipate sehemu ya kujengwa na kuanzia maendeleo ni hapa,” alisema.

Akizungumzia ujenzi huo, Profesa Ndakidemi amesema baada ya ujenzi wa hospitali ya wilaya inayojengwa Mabogini kukamilika na kufunguliwa, wananchi wataweza kupata huduma bora kwa uharaka na kwa unafuu na kuwasaidia kuwapunguzia gharama za matibabu ambazo walikuwa wanazitumia kusafiri zaidi ya kilomita 20 kwenda kupata huduma hizo katika hospitali za Mawenzi na Kibosho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!