Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali: Hakuna mwanafunzi wa Tanzania aliyebaki Ukraine
Habari Mchanganyiko

Serikali: Hakuna mwanafunzi wa Tanzania aliyebaki Ukraine

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imesema hakuna mwanafunzi wa Kitanzania, aliyebaki katika Chuo cha Taifa cha Sumy, nchini Ukraine. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano, tarehe 9 Machi 2022, jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, akielezea jitihada za Tanzania katika kuwoandoa raia wake nchini Ukraine, kulikoibuka vita kati ya taifa hilo na Urusi.

Balozi Mulamula amesema, hatua hiyo imetokana na jitihada za Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ukraine, Urusi na Poland.

“Kwa taarifa tulizonazo hadi sasa, hakuna mwanafunzi kutoka Tanzania aliyebaki kwenye chuo hicho cha taifa cha Sumy nchini Ukraine.

“Kufanikiwa kuodoka kwa wanafunzi hawa kunatokana na jitihada mbalimbali zilziofanwyana Serikali kwa kushirikiana na Ukraine, Urusi na Poland pamoja na mashirika ya kimataifa,” amesema Balozi Mulamula.

Balozi Mulamula, amesema kundi la mwisho la wanafunzi wa Kitanzania 61, liliondoka nchini Ukraine alfajiri ya tarehe 8 Machi mwaka huu, ambapo 50 wanatarajiwa kuingia nchini Hungary na 11 Poland.

Amesema mabalozi wa Tanzania katika nchi za Sweden na Ujerumani, wako kwenye mipaka ya Poland na Hungary, kwa ajili kuwapokea wanafunzi hao watakapofika mipakani.

“Balozi za Tanzania nchini Sweden, Ujerumani na Urusi, zimetoa namba maalumu ili kuwawezesha wanafunzi kuwasiliana na maafisa wa balozi zetu, pindi watakapowasili mipakani,” amesema Balozi Mulamula.

Nchi ya Urusi iliivamia Ukraine tarehe 24 Februari 2022, muda mfupibaada ya Rais wake, Vladimir Putin, kutangaza operesheni ya kijeshi nchini humo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!