Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mfungwa shambulio Septemba 11 arejeshwa nyumbani baada ya miaka 20
Kimataifa

Mfungwa shambulio Septemba 11 arejeshwa nyumbani baada ya miaka 20

Spread the love

MWANAUME mmoja raia wa Saudi Arabia anayetuhumiwa kuwa mtekaji nyara katika shambulio lililofanyika tarehe 11 Septemba 2001ameachiwa kutoka kizuizini katika gereza lenye ulinzi mkali la Guantanamo. Anaripoti mwandishi wetu … (endelea).

Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina la Mohammed Ahmad Qahtani mwenye umri wa miaka 46 amerejeshwa nchini Saud Arabia baada ya bodi ya ukaguzi kubaini kwamba hakuna tena tishio kubwa.

 

Pia bodi hiyo ilibaini hali yake ya kiafya na kiakili imeathiriwa kwa mujibu wa vipimo vya madaktari.

Qahtani aliteswa vibaya na wapelelezi wa Marekani baada ya kuzuiliwa mwaka 2001 kiasi kwamba hakuweza kufikishwa mahakamani.

Bodi ya mapitio ilisema mwezi uliopita kwamba sharti la uhamisho wake linapaswa kuwa ushiriki wake katika kituo cha kurekebisha tabia cha wanajihadi cha Saudi Arabia, kinachojulikana kama Kituo cha Ushauri na Matunzo cha Prince Mohammed Bin Nayef, ambapo anaweza kupata huduma kamili ya afya ya akili.

Mamlaka za Marekani zimedai kuwa Qahtani alikusudiwa kuwa kwenye ndege ya United Airlines ndege namba 93, iliyoanguka Pennsylvania baada ya kutekwa nyara na wanamgambo wanne wa al-Qaeda mnamo 9/11.

Qahtani alikamatwa miezi minne baadaye kwenye mpaka wa Afghanistan na Pakistan na kupelekwa katika kambi ya jeshi la wanamaji la Marekani huko Guantanamo Bay nchini Cuba Februari 2002.

Wachunguzi huko walipokea kibali cha kutumia “mbinu kali zaidi za kuhoji” kwa Qahtani baada ya kukataa mbinu za kawaida.

Kati ya Novemba 2002 na Januari 2003, alitengwa kwa muda mrefu, kunyimwa usingizi, udhalilishaji wa kijinsia na kupigwa na baridi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!