Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wataalam manunuzu ugavi waonywa
Habari Mchanganyiko

Wataalam manunuzu ugavi waonywa

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango
Spread the love

 

NAIBU Katibu Mkuu Wizara wa Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru amesema bado kuna watu ambao sio waaminifu katika Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mafuru ametoa kauli hiyo leo tarehe 9 Machi mwaka huu katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi ya Bodi PSPTB iliyofanyika jijini Dodoma.

Mafuru ambaye amemuwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amesema kupitia taariza za vyombo vya habari na kaguzi mbalimbali, zinaonesha kuna wataalamu wanakiuka maadili ya taaluma.

Kutokana na hali hiyo Mafuru ametoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PSPTB, Jacob Kibona na wajumbe wake kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanaokiuka maadili ya taaluma kwa kuzingatia miiko na maadili ya taaluma ili kuongeza nidhamu katika taaluma hiyo.

“Naomba nitoe wito kwenu mkasimamie sheria iliyoanzisha PSPTB, pia mtambue kuwa wadau wa ununuzi na ugavi wana matumaini makubwa kutoka kwenu kwani nyie mtatoa dira ya chanya katika kutekeleza majukunu yao” ameeleza Mafuru.

Aidha, amesema Bodi hiyo iendelee kutoa wa mafunzo endelevu kwa wataalam na wadau wengine kwenye mnyororo wa ununuzi na ugavi ili kuongeza tija Katika utendaji.

“Pia bodi izingatie kufanya kazi za ushauri zinazohusu taaluma ya ununuzi na ugavi na kusimamia vyema matumizi ya Tehama na mifumo ya kielektroniki katika shughuli za kusajili wataalam.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya PSPTB, Jacob Kibona amesema mambo ambayo yanalengwa kutekekelezwa ni kukamilisha kufanya utafiti wa kitaalam ambao umesimama kwa sababu ya kukosa fedha.

Pia amesema itazingatia taratibu za maadili ya wataalamu wa ununuzi na ugavi, utengenezaji wa mitaala ya kitaaluma, kuandaa agenda za utafiti ambazo zitatumiwa na wataalamu kufanya utafiti za kisayansi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!