Saturday , 4 May 2024
Home Gazeti Habari SAT wapigwa msasa juu ya haki za wanyama
Habari

SAT wapigwa msasa juu ya haki za wanyama

Spread the love

JUMLA ya wafanyakazi 65 wa Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT) wamepewa elimu ya kutambua haki za wanyama hasa wmifugo ili kuweza kusaidia mifugo hiyo kutoa malighafi ambazo ni maziwa, nyama na ngozi iliyo bora. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Mafunzo hayo yalitolewa juzi tarehe 11 Disemba, 2022 katika kituo cha mifugo Vihansi wilayani Mvomero kinachomilikiwa na Shirika hilo lengo likiwa ni kutambua haki muhimu ambazo wanyama hao wanatakiwa kupatiwa kila siku ili kuwa mifugo bora.

Daktari wa mifugo kutoka nchi ya Uganda, Dk. Paul Ssuna alisema wanyama nao wana haki ambazo wafugaji na jamii nzima kwa ujuma wanatakiwa kuzingatia ili kuhakikisha zinafuatwa kwani nijia moja ya kuzalisha mifugo wenye ubora unaokubalika.

“Lengo ni kuona wafugaji wanakuwa na mifugo yenye ubora unaokubalika popote pale duniani hivyo ili kuhakikisha suala hili linatekelezeka wafugaji wote hawana budi kuhakikisha wanyama wanapewa haki zao”alisema Ssuna.

Dk. Ssuna alisema mafunzo hayo yamelenga kuelimisha juu maisha halisi ya wanyama hususan mifugo ambapo alieleza kuwa haki za wanyama ni pamoja na kuishi katika mazingira mazuri kwani kutawasaidia kuonesha sifa zao za asili.

Daktari huo wa mifugo alisema haki nyingine ya wanyama ni kupata maji na chakula cha kutosha, uhuru, kutokuwa na maumivu ambapo aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kusaidia kuielimisha jamii kwa ujumla juu ya haki za wanyama.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo kutoka SAT walisema kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kumhudumia mnyama pale anapoona anatatizo na kwamba watakuwa mabalozi katika kutoa elimu hiyo nchini.

Catherine Aloyce ni miongoni mwa washiriki wa mafunzo hayo alisema awali hakuwa na elimu juu haki za wanyama lakini kutokana na mafunzo hayo amekuwa na uelewa mzuri zaidi ambapo aliahidi kuzielimisha jamii zote hasa za wafugaji.

Naye Mercy Nkya alisema kupitia mafunzo hayo ameweza kutambua haki za wanyama na kwamba shirika lake linahusika na masula ya kilimo na mifugo hivyo mafunzo hayo yamemjengea uwezo wa kutekeleza majukumu yake ya kila siku.

Mkurugenzi Mwenza wa Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania (SAT) Alexander Wostry alisema kuwa mbali na wafanyakazi wa shirika kujengewa uwezo,shirika lake hilo litahakikisha jamii ya wafugaji nchini wanaelimishwa juu ya haki za wanyama ili ufugaji wao uwe na tija kwa taifa.

Wostry alisema kuwa SAT inamiliki kiwanda cha maziwa na kwamba hivi karibuni wataanza kununua maziwa kutoka kwa wafufaji hivyo suala la haki hiyo ni la kuzingatia sana ili malighafi zote zitokanazo na wanyama hao yakiwemo maziwa yawe na ubora unaokubalika kwenye soko la dunia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!