Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari Serikali Zanzibar yawakaribisha wadau wa sheria
HabariHabari Mchanganyiko

Serikali Zanzibar yawakaribisha wadau wa sheria

Spread the love

WADAU wanaojishughulisha na masuala ya utoaji msaada wa kisheria visiwani Zanzibar, wametakiwa kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata haki na wanajua majukumu yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Wito huo umetolewa leo Jumanne, tarehe 13 Desemba 2022 na Makamu wa Pili wa Rais, Hemed Abdullah, akifungua kongamano la kujadili upatikanaji wa haki na namna ya kuboresha huduma za msaada wa kisheria Zanzibar.

Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora visiwani humo, Kwa kushirikiana na Shirika la Legal Services Facility (LSF).

“Niwatake watoaji msaada wa kisheria kufanya kazi zenu Kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ili zilete tija na maendeleo yaliyokusudiwa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Dk. Hussein Mwinyi, imejidhatiti kuhakikisha wananchi wake wanapata haki na wanafuata katiba,” amesema Abdullah.

Aidha, Abdullah amewataka wasaidizi hao kushirikiana na Serikali kutokomeza masuala ya ukatili na unyanyasaji

“Naamini mnafahamu kwamba kwa sasa masuala ya udhalilishaji yamekuwa makubwa katika nchi yetu pamoja na uwepo wa migogoro ya ardhi na usajili wa matukio ya kijamii hususan vyetu vya kuzaliwa. Muendelee kuwa mstari wa mbele kuelimisha wananchi kuungana na Serikali kutokomeza vitendo hivi,” amesema.

Aidha, Abdullah amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia mipaka yao;

“shukrani ziwaendee LSF kwa kutuunga mkono katika ufanikishaji wa jukwaa hili kupitia program ya kuimarisha upatikanaji haki.”

Naya Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, amesema kongamano hilo ni matokeo ya kazi ya shirika hilo chini ya ufadhili wa DANIDA, katika kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya msaada wa kisheria.

“Ni wazi kuwa LSF kupitia ufadhili wa DANIDA imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya msaada wa kisheria na upatikanaji haki katika muongo mmoja uliopita ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar. Mapinduzi haya yameifanya Tanzania kuwa moja ya mifano bora ya kanda ya Afrika inayotolewa na kuxungumzwa ndani na nje ya nchi,” amesema Lulu.

Aidha, Lulu ameiomba Serikali ya Zanzibar, ifanye marekebisho dhidi ya Sheria ya Msaada wa Kisheria ya 2018, ili iweke mazingira bora ya jinsi ya uoatikanaji rasilimali za kuendesha huduma hizo ikiwemo kuweka mfuko wa msaada wa kisheria.

“Ni ukweli usiopingika kuwa ufadhili wa wadau katika sekta hii unazidi kupungua siku hadi siku na hivyo tunapaswa kwa haraka kuangalia jinsi ya kubeba jukumu bila kuathiri ubora na upatikanaji wa huduma bora kwa jamii kabla matumaini ya wanufauka hayajafifia,” amesema Lulu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!