July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Samia awaonya UVCCM, awapa kibarua

Kheri James, Mwenyekiti wa UVCCM

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Samia Suluhu Hassan, amepiga marufuku vitendo vya makada wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), kupanga wagombea kabla ya muda wa uchaguzi kufika. Anaripoti Regina Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Umoja huo unatarajiwa kufanya uchaguzi wa viongozi wake wa kitaifa 2022.

Samia ambaye pia ni Rais wa Tanzania, ametoa marufuku hiyo leo Jumanne, tarehe 15 Juni 2021, akizungumza na vijana jijini Mwanza.

Mwenyekiti huyo wa CCM, amewataka vijana hao waache mara moja vitendo hivyo, badala yake wajikite katika kujenga ajenda zinazohusu maslahi ya kundi hilo nchini.

 

“Sisi CCM tuna uchaguzi mwakani (2022), najua tayari watu wamepiga mahesabu ya kuuza na kunadi wagombea. Sitaki kuona hili linatokea, kama mwenyekiti wa CCM nataka jumuiya ya vijana mjipange vizuri kufanya uchambuzi wa yanayotokea nchini na mtuambie ajenda zenu kwenye hayo ni zipi,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amewataka vijana hao wa CCM, wawe mfano wa kuigwa na vijana wa vyama vingine vya siasa, katika kujadili na kuchambua masuala mbalimbali yanayojitokeza nchini, ikiwemo sera zinazowekwa na Serikali.

“Mkianza ninyi jumuiya nyingine zitafanya, lakini muoneshe njia nyie wa chama change. Naomba jumuiya za vijana kwenye vyama vya siasa nendeni kaangalieni maslahi ya vijana, acheni hii kubeba beba wagomeba,” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!