Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Samia aipa kibarua JWTZ kuelekea chaguzi, aeleza ilivyomweka madarakani
Habari za SiasaTangulizi

Samia aipa kibarua JWTZ kuelekea chaguzi, aeleza ilivyomweka madarakani

Spread the love

AMIRI Jeshi Mkuu wa nchi na Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na vikosi vingine vya ulinzi na usalama, kukaa tayari kukabiliana na chochote kitakachoweza kujitokeza kwenye chaguzi zijazo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akifungua mkutano wa saba wa Mkuu wa Majeshi nchini (CDF), Jacob Mkunda na makanda wa JWTZ, leo tarehe 22 Januari 2024, jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema wito wake huo haumaanishi kwamba nguvu zitumike katika chaguzi hizo, bali vikae sawa kwa kuwa zinashirikisha vyama vingi vya siasa vyenye nia tofauti.

“Ombi langu kwenu ni kwamba mwaka huu na mwakani tunaelekea kwenye chaguzi za nchi yetu, hapa ndipo usalama mkubwa ndani ya nchi unapotakiwa kuangaliwa kwa ukaribu zaidi. Niwaombe sana JWTZ kwenye kamandi zenu tofauti kujipanga kwa sababu tuko wengi chaguzi ambazo zinashirikisha vyama vingi vyenye nia tofauti hatuoni kwamba kila kitu kitakwenda kama kilivyopangwa,”

“Kwa hivyo ni vyema tukakaa tayari kukabiliana na chochote kile kitakachojitokeza. Hatusemi tukafanye chaguzi za kutumia nguvu, hapana. Taratibu, sheria na miongozo ya chaguzi zitafuatwa lakini jeshi na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vikae tayari kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema kuwa, uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 2025 ndio wenye changamoto nyingi, hivyo ameamua kuwapa taarifa mapema ili wajipange.

“Mwakani tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu na ule ndiyo wenye vishindo vikubwa, basi nikasema nitoe tu taarifa na kuwaweka sawa kwamba hayo mambo yanakwenda kutokea na jeshi tuna mchango mkubwa kwenye hayo hatuna budi kujiweka tayari,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia amesema kabla hajakabidhiwa madaraka ya urais alikabiliwa na vipingamizi mbalimbali kutoka serikalini na jeshini, lakini kitendo cha JWTZ kukubali awe Amiri Jeshi Mkuu, kimesaidia kuondoa dhana potofu ya kwamba mwanamke hafai kuwa kiongozi wa nchi.

Alitoa kauli hiyo baada ya kumaliza kupiga picha ya pamoja na viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, pamoja na viongozi wa JWTZ.

“Hii picha imenirudisha kwenye kipaza sauti, moja katika kikwazo kikubwa cha kuweka rais mwanamke Tanzania ilikuwa ni hiki, inakuwaje amiri jeshi mkuu wa jeshi na ilikuwa ni nong’ono kubwa zaidi. Amiri jeshi mwenyewe ana viushungi bwana, sasa inakuwaje lakini siku mliyonivisha kombati hii ikachukuliwa picha watu wakajua kwamba kila kitu kinawezekana na siku hiyo ndio mlijenga imani ya watanzania juu ya mwanamke,” amesema Rais Samia na kuongeza:

“Mengine ya serikalini ni challenge nyingine ambayo unasema mmh kumbe inawezekana, lakini ya jeshi ndiyo ilikuwa challenge kubwa lakini inawezekana.”

Rais Samia ambaye alikuwa makamu wa rais, aliingia madarakani Machi 2021 baada ya mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, kufariki dunia kwa matatizo ya umeme wa moyo alipokuwa madarakani.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!