Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Sakata la uhamiaji Rwanda lamng’oa waziri Uingereza
Kimataifa

Sakata la uhamiaji Rwanda lamng’oa waziri Uingereza

Spread the love

Waziri wa Uhamiaji wa Uingereza, Robert Jenrick amejiuzulu baada ya serikali ya nchi hiyo kuchapisha sheria kuhusu mkataba wenye utata na Rwanda wa kutuma wahamiaji katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Waziri wa Mambo ya Ndani, James Cleverly aliwaambia wabunge jana Jumatano kwamba Robert Jenrick amejiuzulu kwa madai kuwa sheria hiyo ya dharura haijitoshelezi.

“ Sikubaliani na sheria inayopendekezwa kwa sasa kupitia Bunge, kwani siamini kwamba inatupa fursa nzuri zaidi ya kufanikiwa,” ameandika waziri huyo katika barua aliyoielekeza kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak.

Mapema Jumatano Rwanda ilionya kujiondoa katika mkataba wa kuwapokea wahamiaji iwapo Uingereza haitaheshimu sheria za kimataifa.

Uingereza na Rwanda zilitia saini mkataba mpya Jumanne katika jitihada za kufufua pendekezo linaloonekana kuwa na utata la Uingereza la kuwahamisha wahamiaji katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, pendekezo ambalo awali lilipingwa na mahakama ya Uingereza.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza James Cleverly na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Vincent Biruta walitia saini makubaliano hayo mjini Kigali nchini Rwanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Vincent Biruta, ambaye alitia saini mkataba huo wa pande mbili, alisema ukiukaji wowote wa mikataba ya kimataifa unaweza kuifanya Rwanda kujiondoa katika mkataba huo.

Mpango wa Rwanda ni sehemu ya mkakati wa kupunguza idadi ya watu wanaoingia nchini Uingereza kwa kuvuka bahari kwa boti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wanajeshi Ukraine waishiwa risasi, 31,000 wauawa

Spread the loveRais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy amesema zaidi ya wanajeshi 31,000...

Kimataifa

Waziri mkuu Palestina ajiuzulu

Spread the loveWaziri Mkuu wa Palestina, Mohammed Shtayyeh ametangaza kujiuzulu pamoja na...

Kimataifa

Rais mstaafu ahukumiwa miaka 4 jela

Spread the loveMahakama ya mjini Tunis imemhukumu rais wa zamani wa Tunisia,...

Kimataifa

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79 ikiwamo TZ

Spread the loveWaziri wa usalama wa ndani nchini Malawi, Ken Zikhałe ametangaza...

error: Content is protected !!