Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Katesh wapewa lita 14,500 za petroli, dizeli
Habari za Siasa

Katesh wapewa lita 14,500 za petroli, dizeli

Spread the love

Naibu Waziri wa Nishati,Judith Kapinga, kwa Niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amesema Wizara ya Nishati imetoa mafuta lita 14,500 ya petroli na dizeli kwa ajili ya kusaidia na kurahisisha shughuli zinazoendelea katika Mji wa Katesh uliokubwa na janga la maporomoko ya udongo wilayani Hanang Mkoani Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kapinga amesema hay oleo tarehe 7 Desemba, 2023 baada ya kuwasili katika eneo hilo ili kuona uharibifu wa miundombinu ya sekta anayoisimamia ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Magizo la Rais Samia Suluhu Hassan aliyatoa kwa viongozi wote.

Mafuta ya petroli pamoja na dizeli yaliyotolewa ni kwa ajili ya mitambo na magari yanayotumika katika kuondoa matope na magogo katika eneo hilo.

Amesema mafuta hayo yametolewa na Umoja  Makampuni  ya Uagizaji Mafuta  Tanzania (TAOMAC) pamoja na wadau  mbalimbali wanaohusika na sekta hiyo.

Ameomba makampuni hayo na wadau wengine wanaohusika na sekta ya nishati kuendelea kutoa michango  muhimu kwa wananchi hao katika eneo hilo.

Kuhusu nishati ya umeme, Kapinga amesema tayari huduma ya umeme imerejea katika hali yake ya kawaida na zoezi linaloendelea sasa kuunganisha nyumba zilizopata changamoto.

Amesema wamerekebisha mashine 76, nguzo 60 pamoja na njia ya kusafirisha umeme wa msongo mdogo ziliathiriwa na maporomoko hayo.

Katika zoezi hilo Naibu Waziri ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka na viongozi waandamizi kutoka Shirika na Umeme Tanzania (TANESCO).

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA), Charles Mtiesa amekiri kupokea mafuta hayo kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu na mkoa wa Manyara na kusema kuwa watayasimamia na  kuhakikisha mafuta hayo yanatumika kwa shughuli iliyokusudiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!