Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mawakili vijana kufanya matembezi kupinga wenzao kufungiwa
Habari Mchanganyiko

Mawakili vijana kufanya matembezi kupinga wenzao kufungiwa

Edward Heche
Spread the love

CHAMA cha Mawakili Vijana kutoka Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), kimepanga kufanya matembezi ya amani ili kupinga tabia ya wanataaluma hao kufungiwa kufanya kazi kwa kigezo cha ukiukwaji wa maadili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano, Mwenyekiti wa chama hicho, Edward Heche alisema matembezi hayo yatafanyika tarehe 16 Disemba 2023, kuanzia Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, iliyoko Mawasiliano, hadi katika makao makuu ya TLS, jijini Dar es Salaam.

“Sisi mawakili vijana tumepanga kwamba, tutakuwa na matembezi ya amani kutoka Mahakama ya Ufisadi, katika hayo matembezi yetu ya amani tutafanya kuelekea ukumbi wa mikutano lengo kubwa ni kuelezea hisia zetu kuhusu mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanyika kwa kichaka cha kusema kwamba watu wanavunja maadili,” alisema Heche.

Mwenyekiti huyo wa mawakili vijana alisema “lengo letu ni kupeleka ujumbe kuwa hatufurahii kuwafungia mawakili kazi zao kwa kujificha kutoka katika kichaka cha maadili.”

“Naomba nafasi hii tuitumie kikamilifu sababu kesho na kesho kutwa haya masuala yatakuja kutuumiza sisi ambao ndio kwanza tunaanza hii tasnia. Tuitumie nafasi hii kujadili sababu kumkeuwa na matatizo mengi sasa ikitokea sisi ambao watetezi wa haki za watu lakini haki zetu zinavunjwa hatuwezi kujitetea inaibua maswali kwa wananchi kama tutawateteaje wakati sisi hatuwezi kujitetea,” alisema Heche.

Uamuzi huo umekuja siku chache tangu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, kuitaka Kamati ya Maadili ya Mawakili, kuwachukulia hatua mawakili wanaodaiwa kukiuka maadili ya taaluma hiyo.

Kabla ya kauli hiyo ya AG,  wiki kadhaa zilizopita Wakili Mwandamizi, Mpale Mpoki, alisimamishwa kwa muda wa miezi sita na kamati hiyo, akituhumiwa kukiuka maadili wakati akimtetea wakili mwenzake, Boniface Mwabukusi.

Wakili Mwabukusi alifikishwa mbele ya kamati hiyo na ofisi ya AG, kujibu mashtaka yanayomkabili ya ukiukwaji wa maadili na kutoa lugha zsisizofaa kwa viongozi wa Serikali, wakati akijadili sakata la mkataba wa bandari.

Ofisi ya AG imefungua mashtaka hayo ikiiomba kamati hiyo ya maadili imvue uwakili Mwabukusi, kufuatia tuhuma hizo.Hadi sasa kamati hiyo bado haijatoa uamuzi dhidi ya maombi hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!