October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Safari za mabasi usiku zapigwa ‘stop’

Spread the love

JESHI la Polisi limetangaza kusitisha safari za usiku kwa baadhi ya magari ya abiria yanayokwenda mikoani. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

CP Liberatus Sabas, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo amesema, wameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na sababu za kiusalama na kuwa, mabasi yatakayoruhusiwa kufanya safari zake za usiku ni  Morogoro -Dar es Salaam, Shinyanga – Mwanza pekee.

Amesema, mabasi ambayo hayataruhusiwa kufanya safari zake usiku ni Dar es Salaam-Kahama-Mwanza, Dar es Salaam-Tabora-Katavi, Kahama- Geita-Kagera, Kahama kwenda mikoa mingine iliyopo mipakani pamoja na Dar es Salaam-Tabora kwenda katika wilaya zake.

“Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, kulifanyia kazi suala la usalama na baadaye mabasi yote yataruhusiwa kutembea usiku,” amesema.

Kwa mujibu wa CP Sabas ni kwamba, zoezi la kuzuia mabasi hayo kusafiri usiku limeanza kutekelezwa kabla ya taarifa hizo kutolewa.

error: Content is protected !!