December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jezi za Yanga zaanza vizuri, yauzwa kwa laki tano

Spread the love

KLABU ya Yanga imetambulisha jezi za nyumbani na ugenini itakayotumika kwenye michezo ya Ligi Kuu na klabu bingwa Afrika kwa msimu wa 2019/20 kwa upande wa nyumbani na ugenini ambapo jezi ya kwanza ilinunuliwa kwa Sh. 500,000. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa SportPesa Tanzania, Tarimba Abbasi ambaye pia ni mwanachama wa klabu hiyo aliyenunua jezi ya ugenini kwa Sh. 500,000 kutokana na kuvutiwa nayo, amesema kuwa anayofuraha kuona klabu hiyo ikipiga hatua katika mauzo ya jezi.

“Nembo ya Yanga ni nembo kubwa iliyohangaikiwa kwa miaka mingi kuwa hapa ilipo, lakini watu wengi wamefanya mzaha juu ya nembo ya Yanga, nafurahi kuona kuwa sasa ile ndoto niliokuwa nikiifikilia juu ya Yanga hasa vifaa vyake viyakuwa na utaratibu maalumu kwenye kuviuza,” alisema Tarimba.

Baada ya uzinduzi huo, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk. Mshindo Msolwa amesema jezi hizi zitaanza kuuzwa kuanzia leo katika maeneo mbalimbali ndani ya nchi na kuhimiza kuwa ni wakati sasa wa washabiki kuisapoti timu yao.

Yanga anbayo kwa sasa wachezaji wapo kambini mkoani Morogoro inatarajia kucheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya klabu ya Kariobangi Shark kutoka Kenya katika kilele cha siku ya Mwananchi.

error: Content is protected !!