July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jinsi polisi wavyopambana na dawa za kulevya Aprili – Juni 2019

CP Liberatus Sabas, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Polisi

Spread the love

JUMLA ya watu 2,085 wamekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi, kuanzia Aprili hadi Juni 2019. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Takwimu hizo zimetolewa mbele ya wanahabari na CP Liberatus Sabas, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi hilo wakati akizungumzia mafanikio katika misako na operesheni mbalimbali kwenye kipindi hicho.

Amesema, jumla hiyo ya kilogramu 6,446 na gram 132 za dawa hizo za kulevya zimekamatwa katika kipindi hicho.

CP Sabas amesema, katika kipindi hicho, jumla ya kilo 1,312 na gram 156 za mirungu zilikamatwa na watuhumiwa 281 walihusika kwenye mihadarati hiyo.

Amesema, katika kipindi hicho pia jumla ya kilo 10 na gram 5 za dawa za kulevya aina ya Cocaine zilikamatwa na watuhumiwa watatu walihusishwa ambapo kilo 22 na gram 429 za heroine pia  zilikamatwa zikihusisha watuhumiwa 173.

Kwa upande wa kukutwa na silaha pia risasi, CP Sabas amesema, katika kipindi hicho silaha mbalimbali 77 na risasi 5 zilikamatwa zikihusisha watuhumiwa 64.

“Silaha zilizokamatwa ni pamoja na shoti gun 2, pistol 9, Riffle 3 na Gobole 63” amesema.

Kuhusu kupatikana kwa nyara za serikali CP Sabas amesema, katika kipindi hicho jumla ya nyara 899 za wanyama mbalimbali zenye thamani ya Sh. 1.14 bilioni zikijumuisha watuhumiwa 267 zilikamatwa.

“Nyara za serikali ambazo zilikamatwa ni pamoja na ngozi za Chui2, ngozi ya Simba 2, vipande vya meno ya Tembo 551 twiga 2 na nyati 1.

“Makosa ya jinai yamepungua kwa asilimia 1 ukilinganisha na mwaka jana, kutoka makosa 141,847 kwa kipindi cha Aprili-Juni 2018 hadi kufikia makosa 140, 385 kwa kipindi cha Aprili-Juni 2019.

Sabas ameongeza kuwa upande wa matukio ya usalama barabarani yamepungua kwa asilimia 10.9 ambayo ni kutoka matukio 719,258 kwa Aprili-Juni 2018 ukilinganisha na 640,528 yaliyoripotiwa mwaka 2019 ambao ni upungufu wa makosa 78,730.

error: Content is protected !!