Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Sabaya atoa waraka akimlilia Hayati Magufuli
Habari za Siasa

Sabaya atoa waraka akimlilia Hayati Magufuli

Lengai ole Sabaya
Spread the love

 

LENGAI ole Sabaya, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, ameachia “waraka mzito,” ukilenga mustakabali wa maisha yake, baada ya kifo cha Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na Sabaya zinasema, waraka huo, aliuachia siku mbili tokea kufariki dunia kwa Dk. Magufuli aliyekuwa rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk. Magufuli alifariki dunia, saa 12:00 jionitarehe 17 Machi 2021, katika hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam. Alizikwa 26 Machi 2021, nyumbani kwao Chato, mkoani Geita.

Sabaya amesema, usiku wa tarehe 17 Machi, ulikuwa ni usiku mgumu mno kuwahi kumtokea katika maisha yake, na kwamba anaisikitikia siku hiyo kwa kuwa amempoteza mtu mwenye upendo ana “anayehukumu baada ya kusikiliza.”

Anaongeza, “…nimempoteza Baba, Mwalimu na mtu mwenye huruma, ambaye kabla ya ‘kukuhukumu’ atataka na wewe akusikilize na siku zote akisema usiogope. Mtu asiyejua unafiki wa kupikwa.”

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema, pamoja na kwamba waraka wa Sabaya kwa Dk. Magufuli, uliandikwa kabla ya mwanasiasa huyo hajaingia matatani, lakini ujumbe uliyomo kwenye waraka huo, unaweza kuwa na uhusiano mkubwa na pengine wa moja kwa moja na matatizo anayopitia sasa.

Undani wa waraka huo na uchambuzi wa kina wa alichokisema Sabaya ambaye sasa yuko gerezani, soma Gazeti la Raia Mwema, la leo Jumanne, tarehe 15 Juni 2021.

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!