Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Mgombea Urais aibua hoja ya ushiriki wa Zanzibar uchaguzi TFF
Michezo

Mgombea Urais aibua hoja ya ushiriki wa Zanzibar uchaguzi TFF

Spread the love

Ali Saleh ‘Alberto’ moja ya wagombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ameibuka na hoja ya ushiriki wa Zanzibar katika uchaguzi huo kutokana na kutopewa nafasi ya kudhamini wagombea. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mgombea huyo ameibua hoja hiyo jana, kwenye mkutano wake na waandishi wa habari katika kuelekea uchaguzi mkuu wa Tff utakaofanyika tarehe 8 Agosti 2021.

Katika maelezo yake Ali Saleh alisema kuwa ameandika barua kwenda kwa msajili wa vyama vya michezo, huku kukiwemo na hoja ya ushiriki wa Zanzibar kwenye uchaguzio huo licha ya kanuni kutowatambua katika kuwadhamini wagombea wa nafasi tofauti.

Ali Saleh alifunguka kuwa kuna haja sasa ya kuhoji muundo wa Shirikisho hilo kwa kuwa ushiriki wa Zanzibar ni finyu licha ya Tff kusimamia mpira Tanzania Bara na Visiwani.

“Kwa mujibu wa katiba ya Tff, wanachama wa shirikisho hilo ni klabu kutoka bara na vyama vya mikoa kutoka bara, lakini chombo hiki kinatakiwa kusiamia soka la Tanzania.”

“Lakini mimi au mzanzibar hasingeweza kupata haki ya kudhaminiwa na  wazamini kutoka bara, na vile kuna ulazima gani wa kufanya uchaguzi wa chombo unachokiita kutoka Tanzania na kinanyima haki wanzabar.” Alisema mgombea huyo

Aidha katika hatua hatua nyingine mgombea huyo alisema kuwa, swala la wadhamini limetengenezwa kama mpango wakuwanyima wengine fursa kwenye uchaguzi huo licha ya kuwepo kwenye kanuni.

“Udhamini (Indorsement)umetengenezwa kama mpango mkakati mwaka mmoja uliopita, kwa sababu walijua nini kitatokea baada ya mwaka mmoja ukifika uchaguzi.” Alisisitiza Alberto

Badhi ya malalamiko mengine yaliyokuwa kwenye barua ya mgombea huyo ni pamoja na kuwepo kwa kipindi kifupi cha zoezi la uchukuaji na urudishwaji wa fomu pamoja na kutafuta wadhamini, limefanyika ndani ya kipindi kifupi cha siku nne, jambo ambalo halikutosha kukamilisha taratibu za kupata wadhamini kwa nchi nzima.

“katika kipindi hiko cha muda mfupi ilikuwa ngumu kwa wagombea hao wanafasi ya urasi, kudhaminiwa kutokana na kuhitajika kufanyika kwa vikao vya kamati tendaji za mikoa, klabu na vyama washirika wa Tff ambao ndio wadhamini wanaotambulika kisheria kwenye mchakatao huo.” Aliandika Ali Salehe

Katika hatua nyingine ya kuwasilisha malalamiko hayo kwa msajili wa michezo Ali Saleh alieleza kuwa, katiba ya sasa ya Tff, inatambua klabu za Ligi Kuu kuwa ni 16, badala ya 18 ambavyo ni wanachama mpaka sasa.

Kwa mantiki hiyo Ali Saleh kwenye barua yake ameeleza kuwa klabu mbili hazikuwa na haki ya kumdhamini mgombea yoyote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!