Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa RC Mongela awaaga 818 wanaohama Ngorongoro
Habari za Siasa

RC Mongela awaaga 818 wanaohama Ngorongoro

Spread the love

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amewahakikishia wananchi wanaohama kwa hiari kutoka ndani ya hifadhi ya Ngorongoro kwenda maeneo mengine nje ya hifadhi kuwa serikali imejipanga na hakuna mwananchi yoyote atakayekosa haki zake iwapo ataamua kuhama kwa hiyari. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mongella ametoa kauli hiyo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha leo tarehe 25 Januari, 2024 wakati akiwaaga wananchi 818 walioamua kuhama kwa hiyari kutoka ndani ya hifadhi hiyo na kwenda kuishi katika Kijiji cha Msomera wilayani Handeni Mkoani Tanga.

Ameeleza kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha za kutosha ili kuhakikisha kuwa zoezi hilo linafanikiwa na hakuna mwananchi yoyote atakayekosa kulipwa haki zake zote zilizoanishiwa katika utekelezaji wa zoezi hilo.

Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa zoezi hilo linatekelezwa kwa kuzingatia misingi yote ya haki za binadamu ikiwemo kuboresha maisha ya wananchi hao wanapofika katika Kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga.

Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Richard Kiiza amesema kumekuwa na muamko na ari kubwa ya wananchi kujiandikisha na kutaka kuhama kwa hiyari ambapo  katika  tukio hilo jumla ya kaya 118 zenye watu  818 na mifugo  3,129 wamehama kwenda Kijiji cha Msomera.

Mratibu wa zoezi hilo la kuhamisha watu kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, Fedes Mdalla amesema uhamisishaji wa wananchi kuhama ndani ya hifadhi unaendelea na zoezi hilo litakuwa linafanyika kila mara kulingana na idadi ya nyumba zinazoendelea kujengwa na kukamilika katika eneo la mradi.

Baadhi ya wananchi walioamua kuhama kwa hiyari kwenda katika Kijiji hicho wameishukuru serikali kutokana na jinsi inavyozingatia utu na maslahi ya kila mmoja katika kuhakikisha kuwa wanapata stahiki zao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao Sindato Ngenyike na Theresia Moko wamesema kitendo cha wao kuondoka ndani ya hifadhi kimetokana na elimu waliyoipata  kutoka kwa serikali na wananchi wenzao ambao tayari wameshamia katika Kijiji cha Msomera.

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro inaendelea kuelimisha, kuandikisha na kuhamisha wananchi kutoka ndani ya hifadhi hiyo kila wiki ikiwa ni zoezi lenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi na pia kulinda na kuimarisha hifadhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!