JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Indonesia zimesaini mikataba minne ya ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).
Mikataba hiyo imesainiwa leo tarehe 25 Januari 2024, jijini Jakarta nchini Indonesia mbele ya Rais wa taifa hilo, Joko Widodo na Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye yuko katika ziara ya kikazi kuanzia jana hadi tarehe 26 Januari mwaka huu.
Mikataba iliyosainiwa ni ya ushirikiano katika ukuzaji ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Indonesia, sekta ya kilimo, madini, uchumi wa buluu hususan kwenye uvuvi na usafiri wa majini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia alisema mikataba hayo ni matokeo ya pande zote mbili kuridhishwa na makubaliano yaliyowekwa Agosti 2023 Rais Widodo alipowasili Tanzania kwa ziara ya kikazi.
“Tulijadili ujio wa Rais Widodo Agosti 2023 na kuridhishwa na utekelezaji wa maazimio tuliyokubaliana pande zote mbili na kukubalia kuongeza zaidi utekelezaji. Tumesisitiza kuendelea kushirikiana kukuza ushirikiano katika uwekezaji baina ya nchi zetu mbili na baadae nitashiriki jukwa la biashara kati ya jumuita ya wafanyabiashara wa Indonesia na Tanzania,” amesema Rais Samia.
Leave a comment